• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Mabeyo Achangisha Zaidi ya Milioni 40 Kujenga Nyumba ya Mapadre Jimboni Rulenge Ngara Mkoani Kagera

Imewekwa : September 8th, 2019

Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo ashiriki na kuendesha harambee ya ujenzi wa nyumba ya  Mapadre wa Parokia ya Mtakatifu Francisco wa Assiz Jimbo Katoriki la Rulenge Ngara  Mkoani Kagera ambapo pamoja na kuchangia ujenzi huo lakini pia aliwaongoza na kuwahamasisha waamini wa jimbo hilo kuchangia ujenzi huo.

Akiwakilishwa na Lt.  Jenerali Mnadhimu Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Samwel Ndomba katika harambee hiyo iliyofanyika katika viwanja vya ofisi za Baba Askofu wa Jimbo Katoriki la Rulenge Ngara Seveline Niwemugizi Septemba 8, 2019 Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo alichangia kiasi cha shilingi milioni kumi na kuchangisha jumla ya shilingi milioni arobaini taslimu na ahadi katika harambee hiyo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akimuunga mkono Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Mabeyo katika harambee hiyo alichangia shilingi milioni kumi taslimu na kusema kuwa nyumba hiyo si ya Mapadre tu bali ya viongozi mbalimbali wa nchi ambao wanaweza kusema neno kwa wananchi  na mkoa ukasonga mbele kwa maendeleo hasa kwa kupunguza mauaji katika jamii.

Awali kabla ya harambee hiyo mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi nchini Lt. Jenerali Mstaafu Ndomba alishiriki katika ibada takatifu iliyongozwa na Askofu wa Jimbo Katoriki la Rulenge Ngara Seveline Niwemugizi katika Parokia ya Mtakatifu  Francisco wa Assiz Ngara ambapo aliweza kutoa ujumbe kwa waamini wa kanisa hilo kuchangia ujenzi wa nyumba za Mapadre katika Parokia hiyo.

Lt. Jenerali Mstaafu Ndomba ndani ya Kanisa aliwakumbusha waamini kuwa ni heri kumtolea Mwenyezi Mungu mchango kabla yeye mwenyewe hajaamua kujichukulia. “Baadhi ya waamini hujifikiria mara mbili kutoa michango au hutoa chenji badala ya kutoa kitu kizima lakini hewa safi tuvuta bure wote hapa wakati kuna wagonjwa hospitalini wanaivuta kwa kulipia  gharama kubwa na hili ni angalizo kwetu kutoa michango kujenga kanisa la bwana.” Alisisitiza Lt. Jenerali Mstaafu Ndomba.

Lt. Jenerali Mstaafu Ndomba alitolea mfano wa Makanisa ya Ulaya kuwa kwasasa makanisa hayo wamebakia waamini wazee tu vijana hawaendi tena kanisani na wakati huo huo Afrika Makanisa yanazidi kujaa waamini na sababu kubwa ni Makanisa hayo kutoa huduma mbalimbali za kiroho na kijamii kama elimu na afya na kuwagusa vijana walio wengi na kuamua kumfuata Kristo.

Naye Askofu Seveline Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara akiongoza ibada hiyo ya harambee aliwakumbusha waamini kuwa wafuasi halisi wa Kristo na wasiwe mashabiki tu ambao hupenda kusikiliza mtu anaongea nini na kuishia hapo,  bali wabebe msalaba wa kweli kwa kushiriki na kuchangia michango mbalimbali kama wanafunzi wa Yesu walivyojitoa na kuwa wafuasi wa kweli na si mashabiki.

“Tumekuwa tukieneza injili na kuombea miito na vijana wameitikia wito kweli kweli, hivi juzi tulikuwa katika kikao cha bodi ya Seminari zetu kuu tano nchini ambazo ni Segerea, Kipalapala, Ntungamo, Kibosho na Peramiho vijana wetu sasa hawana pa kukaa, sasa sisi waamini lazima tubebe msalaba wa kuwapatia mahala pa kuishi kwa kuchangia ujenzi wa nyumba mpya au upanuzi wa zilizopo.” Alisisitiza juu ya michango Askofu Niwemugizi.

Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francisco wa Assiz Ngara Padre Sixmund Nyabenda aliwakumbusha waamini kuwa wamisionari waliokuwa wakitoa michango ya ujenzi wa kanisa la Mungu hawapo tena na kama wapo huko nchi za Ulaya wapo katika vyumba vya wagonjwa mahututi na akasema wamisionari ni waamini wenyewe wa kujenga kanisa la Mungu.

Ujenzi wa nyumba ya Mapadre Parokia ya Mtakatifu Francisco wa Assiz Ngara unahitaji kiasi cha shilingi milioni 400 na inatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka mitatu. Aidha, katika harambee hiyo mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi nchini Lt. Jenerali Mstaafu Ndomba aliweza kuchangisha zaidi ya shilingi milioni 30 taslimu na ahadi zaidi ya shilingi milioni 10.5 ikiwa ni pamoja na vifaa vya ujenzi ambavyo ni saruji mifuko 95.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa