• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Awachukulia Hatua Wasimamizi wa Miradi ya Ukarabati wa Shule Kongwe Kwa Uzembe Ampiga Stop Mkandarasi wa Barabara Manispaa ya Bukoba Kutotoka Nje ya Mkoa

Imewekwa : November 21st, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi kuwaweka chini ya ulinzi wasimamizi wa miradi ya ukarabati wa Shule kongwe katika Manispaa ya Bukoba baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo na kutoridhishwa na kasi ya maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo wakati Serikali ilishatoa fedha zote za ukarabati kila shule.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alichukua hatua hiyo Septemba 21, 2019 wakati wa ziara yake Manispaa ya Bukoba katika Shule kongwe za Kahororo, Rugambwa, Kagemu na Bukoba ambazo kwa pamoja zilipewa jumla ya shilingi bilioni 2,595,890,485.33 na Serikali kufanya ukarabati wa majengo ili kuzirejesha shule hizo katika hali nzuri lakini pamoja fedha hizo kuingizwa katika kila akaunti ya shule husika ukarabati umechukua muda mrefu au kuendelea kwa kusuasua na kupitiliza muda uliotolewa na Serikali kukamilika.

Baada ya kufika katika Shule ya Sekondari Kahororo na kutoridhishwa na ukarabati unaoendelea kwa kudorora pia kutoridhishwa na maelezo ya mkandarasi ambaye ni Mzinga Holding Company alimwelekeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi kuwaweka chini ya ulinzi Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Marck Ogambage kwa uzembe wa usimamizi pamoja na Mhandisi Festo Talimo wa Mzinga kwa kufanya kazi kwa uzembe lakini pia Afisa Manunuzi wa Manispaa ya Bukoba Batreth Rwiguza kwa kufanya kizembe mchakato wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi.

Wengine waliochukuliwa hatua kwa uzembe huo ni pamoja na Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Bukoba George Geofrey   kutosimamia ipasavyo ukarabatihuo aidha,  katika Shule ya Sekondari Bukoba Kaimu Mkuu wa Shule Mwalimu Siasa Phocus pia alichukuliwa hatua kwa kuzembea kusimamia ukarabati wa shule hiyo huku zaidi ya milioni 900 zikiwa zimeishatumika kati ya Shilingi bilioni 1,481,701,194.33 zilizotolewa na Serikali kuhakikisha shule hiyo inarudi katika hali nzuri.

Shule ya Sekondari Kagemu ilipewa na Serikali Shilingi milioni 152,000,000 tayari muda wa ukarabati umeisha na zimelipwa milioni 49,485,277.22 Shule ya Sekondari Kahororo ilipewa na Serikali shilingi milioni 893,883,994 kati ya hizo zimetumika  shilingi milioni 297,966,594.96 muda wa ukarabati ukiwa umeisha bila kazi kukamilika. Shule ya Sekondari Rugambwa ilipewa shilingi milioni 872,800,297 na zilizotumika ni shilingi milioni 275,125,889.25 ambapo muda wa ukarabati ukiwa umeisha.

Mradi wa Barabara 

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alitembelea na kukagua mradi wa barabara wa kilometa tano unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kujengwa katika Manispaa ya Bukoba wenye thamani ya shilingi bilioni 7.3 ambapo hakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya JASCO Building and Civil Engineering Contractors ya Jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alimweleza Mkandarasi huyo kuwa mradi unasuasua na asilimia ya ujenzi ni 40 tu wakati alitakiwa awe amevuka hapo ambapo alimwagiza kutotoka nje ya mkoa hadi atakapohakikisha kuwa mradi huo unaendlea vizuri. Aidha, alimweleza mkandarasi huyo kuhakikisha fedha anazolipwa na Manispaa ya Bukoba kutekeleza mradi wa Bukoba na siyo kuhamisha fedha kwenda kutekeleza miradi  aliyonayo  katika mikoa mingine.

“Nilikuwa nimezuia malipo yako kwasababu nimefuatilia na kugundua kuwa ukilipwa fedha hapa unapeleka kwingine kumalizia miradi ya sehemu nyingine sasa fedha za mradi huu zitalipwa kwenye akaunti ya Bukoba na nitaviagiza vyombo vyangu kuhakikisha fedha hizo zinafanya kazi ya Bukoba na si vinginevyo.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Mwisho Mhe. Gaguti alimweza Mkandarasi huyo wa  Kampuni ya JASCO kuhakikisha anawalipa wafanyakazi wake na pasiwepo kna mtu yeyeyote anayemdai wakati Manispaa ya Bukoba inamlipa fedha za kutekeleza mradi huo kwa wakati. Akimalizia ziara yake Mhe. Gaguti aliwaeleza watendaji hasa wanaopewa jukumu la kusimamia miradi wahakikishe wanatekeleza wajibu wao kwa uzalendo kwani Serikali imetoa fedha zote ili miradi ikamilike kwa wakati.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa