• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Awaongoza TRA Kagera Kutoa Elimu ya Kodi Mitaani Ili Kufikia Lengo la Kukusanya Kodi Kwa Asilimia Mia Moja Mwaka 2019

Imewekwa : March 1st, 2019

Katika kuhakikisha azma yake ya kuufanya Mkoa wa Kagera unakuwa kinara katika ukusanyaji wa kodi kwa asilimia 100% kama ambavyo alitangaza mwezi Januari 11, 2019 kuwa mwaka 2019 utakuwa mwaka wa Kodi Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera  akishirikiana na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani  Kagera apita mitaani kwa Wafanyabiashara katika Manispaa ya Bukoba na kuwaelimisha juu ya kutumia mashine za Kielektroniki za kutolea risiti (EFD)

Februari 28, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti na Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntoga pamoja na maafisa wengine walipita kwa wafanyabiashara katika mitaa ya Rwamishenye, Kashai Mafumbo na Soko Kuu (almaarufu kama SENATE) kwa kutembelea baadhi ya maduka na kutoa elimu kwa wafanyabiashara ambao biashara zao zinaonesha kuwa wanatakiwa kuwa na mashine za EFD lakini hawana.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alikuwa akiwaelimisha wafanyabiashara hao kuwa ni muhimu sana kutumia mashine hizo kwa kutoa risiti kwani Serikali inakosa mapato kutokana na wao kukwepa kuzitumia mashine za EFD ambapo kupitia kodi hizo zinazokusanywa ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kutolea huduma mbalimbali za kijamii kama barabara, shule, Hospitali pamoja na kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi.

Baadhi ya wafanyabiashara waliotembelewa walikutwa wanao uwezo wa kuwa na mashine za EFD kutokana na biashara zao zinavyoonekana pia na wao wenyewe kukiri kwa vinywa vyao kiasi cha fedha wanchoingiza kwa  mauzo ya siku lakini hawana mashine hizo bali wana vitabu vya risiti ambavyo navyo hawavitumii ipasavyo kutoa risiti kwa wateja wao wanaowauzia bidhaa mbalimbali.

Mfano mama Faima Sylvester mfanyabiashara ya vifaa vya shule katika mtaa wa Rwamishenye alikutwa hana mashine ya EFD lakini alikuwa na kitabu cha kutolea risiti ambacho tangu mwaka 2016 alikuwa ametumia kurasa kama tatu tu hadi mwaka huu 2019. Baada ya kuelimishwa na Mkuu wa Mkoa na timu yake alikiri kuwa baada ya wiki moja atakuwa ameshughulika na kupata mashine hiyo ya EFD ili akadiriwe vizuri baishara yake na TRA.

Akiwa Soko Kuu la Bukoba Senate Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaelimisha pia wananchi waliohudhuria kumsikiliza kuwa ni wajibu wao kuomba risiti pale wanaponunua bidhaa mbalimbali madukani. Pia alitolea mfano wa Bwana mmoja aliyekamatwa na alikuwepo mbele ya wananchi akisafirisha nondo, saruji na baadhi ya vifaa vingine vya ujenzi bila kuwa na risiti ya dukani alikonunua vifaa hivyo.

Naye Bw. Adam Ntoga Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera katika kuwaelimisha wafanyabiashara alikuwa anawaeleza kuwa kwa kila mfanyabiashara anayeingiza kiasi cha shilingi 39,000/= kwa siku na kwa mwaka ni zaidi ya shilingi  milioni 14 anatakiwa kuwa na mashine ya kielektroniki ya kutolea risiti EFD.

Aidha, Bw. Ntoga aliwaeleza wafanyabiashara kuwa mashine za EFD zinatolewa bure na Serikali lakini mfanyabiashara anatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 590,000/= mwanzoni na baada ya TRA kumkadiria kodi anayotakiwa kulipa kwa mwaka fedha hizo zinarejeshwa kwa njia ya kutokatwa kwenye kodi ambayo atakuwa amekadiriwa.

Ikumbukwe kuwa ni wajibu na haki ya kila mwananchi kudai risiti kila akinunua bidhaa yoyote na mfanyabishara anawajibu wa kutoa risiti tena yenye thamani halisi ya kiwango cha fedha zilizonunua bidhaa hizo. Aidha, mwananchi ukikamatwa na bidhaa yoyote ambayo umeinunua na huna rsisti yake utawajibishwa kwa mujibu wa sheria kwa kukwepa kodi ya Serikali lakini pia bidhaa hiyo inaweza kukuweka matatani kuwa ya wizi.

Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera kama zikitiliwa maanani na wananchi na wafanyabiashara na kujenga utamaduni wa kulipa kodi au kudai risiti ndio chanzo cha mkoa kupiga hatua kubwa za maendeleo kwani fedha za kodi zitawasaidia wananchi katika kuwaletea huduma karibu kutoka katika Serikali yao.

Mfano mzuri ni Mkoa wa Kagera sasa tayari umepewa fedha bilioni 4.5 bilioni 1.5 kila Wilaya  kwa Wilaya za Bukoba, Karagwe na Kyerwa kujenga Hospitali za Wilaya na tayari ujenzi umeanza na unaendelea. Pili Serikali imetoa bilioni 1.4 kuikarabati Shule ya Sekondari Bukoba (Maarufu kama Bukoba Sec) katika Manispaa ya Bukoba. Tatu Serikali imetoa bilioni 5.9 na kujenga vituo 14 vya afya katika maeneo mbalimbali Mkoani Kagera hizo zote ni kodi za wananchi.

Wito wa Mkoa wa Kagera ni ewe mfanyabiashara lipa kodi kwa manufaa ya mkoa wako na ustawi wa nchi yetu. Serikali ya Awamu ya Tano sasa imeamua kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia kodi zao lakini kodi rafiki ambayo haimbugudhi mfanyabiashara bali kumfanya naye apige hatua kutoka pale alipo na kusonga mbele bila kufungiwa biashara zake bali kwa kuelimishwa na kuelekezwa.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa