- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa Bw. Albert John Chalamila aendelea na ziara ya kujitambulisha na kukagua miradi ya maendeleo, kutembelea na kuongea na Makarani wa Sensa katika Halmashauri za Wilaya za Ngara na Biharamulo Mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa Chalamila akiwa Wilayani Biharamulo Agosti 16, 2022 alitembelea mradi wa maegesho ya magari makubwa (Malori ya mizigo) Nyakanazi uliojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni... na kuongea na wananchi wa eneo hilo ambapo amewahaidi wananchi hao kutatua changamoto ufinyu wa ardhi ili wapate maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo yao.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Chalamila alitembelea vituo vya mafunzo ya Makarani wa Sensa na kuongea na Makarani hao kwa kuwaasa kuzingatia mafunzo wanayopatiwa na wakufunzi ili muda utakapofika Agosti 23, 2022 watekeleze jukumu lao kwa umakini, usiri na uzalendo wa hali ya juu ili kupata takwimu sahihi za sensa kwa kwa mkoa wa Kagera kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania.
Katika ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa Chalamila alikutana na kuongea na Madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuo na kuwaasa kufanya kazi kwa ushirikiano hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi na watumishi kupendana na kutunza siri za Serikali katika maeneo yao ya kazi.
"Mimi huwa nawashangaa baadhi ya Madiwani utasikia wanasema sisi hatumtaki mtumishi fulani au Mkurugenzi wa Halmashauri na wakati mwingine tunapokuwa na Viongozi wa kitaifa Diwani anasimamishwa badala ya kusemea maendeleo ya wananchi wake yeye anatumia muda kusema simtaki Mtendaji wa Kata, huo siyo uongozi bali uongozi ni kurekebishana sisi wenyewe ndani". Alisistiza Mkuu wa mkoa Chalamila
Akihitimisha ziara yake Wilayani Biharamulo Mkuu wa Mkoa Chalamila alitembelea na kukagua mradi wa maji Biharamulo mjini uliofikia aslimia 98 ya utekelezwaji na uliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 450,234,0000 na Mkandarasi (Nakatech Construction Company Ltd) mbapo aliagiza mradi huo kukamilika kwa asilimia 100 kwa muda uliopangwa Septemba 15, 2022 na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa