• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Gaguti Aweka Jiwe la Msingi Katika Mradi wa Ujenzi wa Barabara wa Shilingi Bilioni 7.3 Manispaa ya Bukoba

Imewekwa : August 23rd, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Marco E. Gaguti aweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami nzito zenye urefu wa kilometa tano katika Manispaa ya Bukoba ambapo mradi huo utagharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 utakapokamilika Mwezi April 2019.

Mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la mradi Nshambya kwenye kipande cha barabara chenye kilometa 1.7 Mkuu wa Mkoa Gaguti alimtaka Mkandarasi NCL INTERNATIONAL LIMITED kutekeleza mradi huo kwa kiwango kinachotakiwa na kuukamilisha kwa muda uliopangwa au ikiwezekana aukamilishe kabla ya muda ili wananchi wawanufaike na mradi huo mapema zaidi.

Pia Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanausimamia mradi huo pamoja na kuwa na wasimamizi wataalamu lakini pia wananchi wana wajibu wa kutoa taarifa  watakapoona hawaridhishwi na kazi zinazotekelezwa na Mkandarasi watoe taarifa mara moja kwani mwisho wa siku mradi huo utabaki kuwa wa kwao na ndio wanufaika.

Vilevile Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuwahasa wananchi katika mambo makuu mawili ya msingi ambapo jambo la kwanza aliwaasa kufanya kazi kwa bidii sana ili kujiingizia kipato. Aidha, Mhe. Gaguti aliwahakikishia wananchi kuwa atashughulikia kero wajasiliamali mbalimbali hasa Waendesha pikipiki (Maarufu Bodaboda) ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na kulipa kodi za Serikali.

Jambo la pili alilowaasa wananchi ni kuwa atahakikisha anasimamia  kwa karibu sana ulipwaji wa  kodi za Serikali kwa kila anayetakiwa kulipa iwe mwananchi mmoja mmoja,Taasisi au Kampuni ili Mkoa wa Kagera uweze kuongoza katika ulipaji wa kodi za Serikali kama unavyoongoza kwa kushika nafasi za juu katika elimu ili fedha hizo zirejeshwe na kufanya shughuli za maendeleo ya wananchi.

Mradi wa ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Bukoba umegawanyika katika sehemu kuu nne ili kukamilisha kilometa tano ambapo kilometa 1.7 ni barabara ya Nshambya KCDP itakayogharimu zaidi ya  shilingi bilioni 2.1 Aidha, kuna kipande cha Show kilometa 1.05, Nyangoye kupita Halmashauri ya Bukoba (Chemba) kilometa 1.3 na kipande cha kilometa 1.95 cha Bin Said hadi Kilimahewa. Barabara zote zenye urefu wa jumla ya kilometa 5 zitagharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3

Fedha za kutekeleza mradi huo wa kuimarisha miundombinu ya barabara mijini ilitolewa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo muda wa utekelezaji wa mradi ni kuanzia Juni 18, 2018 hadi Aprili 17, 2019 ambapo kazi ziatakazofanyika ni kujenga makaravati 17, mifereji ya maji, kuweka rami nzito na kujenga daraja moja eneo la barabara ya kuelekea ziwani.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkao Gaguti alitembelea kiwanda cha BUKOP cha kukoboa kahawa kujionea ukoboaji wa kahawa unavyoendelea, Pia litembelea mradi wa BUWASA wa upanuzi wa huduma za maji Ihungo  na kukagua Ujenzi wa madarasa yaliyofadhiliwa na Serikali ya Watu wa Japani katika Shule za Msingi Kashozi na Nyakato Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, mwisho aliongea na kujitambulisha kwa watumisha wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoba na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ukumbi wa chemba Bukoba Vijijini.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa