• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Kagera Aja na Kampeini ya Siku Tatu ya Msaada wa Kisheria Kwa Wananwake Kutatua Kero Zao Zote za Unyanyaswaji

Imewekwa : June 21st, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kuwakomboa wanawake ambao wamehangaika kwa muda mrefu kwa matatizo ya kunyanyaswa kijinsia, kudhurumiwa ardhi, migogoro ya mirathi, na kutelekezewa watoto ambapo ametenga siku tatu kufanya kampeini itakayojulikana kama “KAMPEINI YA MSAADA WA KISHERAI KWA WANAWAKE”  kwa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao ndani ya siku tatu hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Gaguti akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake Juni 21, 2019 alisema katika mkoa wa Kagera kero nyingi ni za ardhi lakini pia wanawake wamekuwa wakipata matatizo makubwa upande wa ardhi, mirathi, kunyanyaswa kijinsia pia kutelekezewa watoto jambo ambalo linawafanya wengi wao kufika mara kwa mara ofisini kwakwe kuwasilisha malalamikoa yao.

Kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa sasa ameamua kutenga siku tatu za Kapeini ya msaada wa Kisheria kwa wananwake  kuanzia tarehe 27 hadi 29 Juni, 2019 kuwasikiliza wanawake  na kutatua kero zao kwa kuzihusisha Idara na Taasisi zote za Serikali na zisizokuwa za Serikali zinazohusika katika usaidizi wa kisheria au zinazojihusisha na ustawi wa jamii.

“Badala ya mama kuja ofisini kwangu alafu niwaite wataalamu wa kunisaidi kusikiliza matatizo na kunishauri au kumtuma mama huyo kuangaika katika ofisi nyingine nimeamua kuwaleta Wataalam wote pamoja ili watoe utatuzi wa kero za wanawake kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na ushauri wa nini mwanamke au mama  aliye na kero afanye nini  ili kero  yake lifike mwisho.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Katika Kampeini hiyo ya Msaada wa Kisheria kwa Kanawake Mkoani Kagera patakuwepo na Wanasheria zaidi ya 15 ikiwa ni pamajo na wanaotoka Shirika la MHOLA linalojihusisha na usaidizi wa kisheria kwa wanawake, Maafisa wa Polisi Kutoka Dawati la Jinsia, Maafisa Wapelelezi kutoka Jeshi la Polisi, Maafisa Kutoka TAKUKURU pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kuhakikisha kila kero imepatiwa ufumbuzi.

Kampeini hiyo ya siku tatu ya Msaada wa Kisheria kwa Wanawake itatolewa bure bila gharama yoyote na  itafanyika Viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba tarehe 27 hadi 29  Juni, 2019 kuanzia saa 2:00 asubuhi kila siku kwa siku hizo tatu na  itafanyika kwa mfumo wa kielektroniki ili kuweka kumbukumbu sahihi juu ya utatuaji wa kero za wananchi.

Wito wa Mkuu wa Mkoa Gaguti kwa wanawake Mkoani Kagera ni kujitokeza kwa wingi kuleta kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi lakini pia akina baba haswa wanaonyanyaswa kijinsia pia nao wanakaribishwa kusikilizwa ili kero zao zitatuliwe pamoja na mwananchi yeyeyote mwenye kero yake anaombwa kuwasilisha ndani ya siku tatu zilizotajwa ili zipatiwe ufumbuzi.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa