• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Kijuu na Katibu Tawala Mkoa CP Diwani Athuman Wakishiriki Hatua za Kupata Pasipoti ya Kielekitroniki

Imewekwa : June 8th, 2018

Pasipoti za Kielekitroniki Zazinduliwa Rasmi Mkoani Kagera na Kutolewa Kwa Mara ya Kwanza Kwa Wananchi wa Kagera

Mkoa wa Kagera wazindua Rasmi Pasipoti za Kielekitroniki leo Juni 8, 2018 katika viwanja vya Uhuru Manispaa ya Bukoba ambapo Pasipoti hizo zimezinduliwa na kutolewa kwa mara ya kwanza  Mkoani Kagera kwa Viongozi na Wananchi wa kawaida na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mkuu wa wa Wilaya ya Bukoba  Mhe. Deodatus Kinawilo.

Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu  Mhe Deodatus Kinawilo akizindua Pasipoti za Kielekitroniki katika viwanja vya Uhuru alisema kuwa Mkoa wa Kagera unajivunia kuzindua wa  Pasipoti za Kielekitroniki  kwani sasa wananchi wake watapata Pasipoti zinazotambulika Kimataifa na zenye uhakikaka zaidi.

Mhe. Kinawilo alisema kuwa Pasipoti ya Kielekitroniki inayo mambo muhimu makuu manne tofauti na Pasipoti  ya zamani kama ifuatavyo; Kwanza, Ni pasipoti inyomtambulisha Mtanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kimataifa,  kwahiyo Pasipoti ya Afrika Mashariki haitatolewa tena bali itatumika Pasipoti  moja ya Kielekitroniki tu.

Pili, Pasipoti ya Kielekitroniki inazo alama za kiusalama ambazo si rahisi kuzigushi. Tatu, Pasipoti ya Kielekitroniki ni ya Kimataifa ambayo hahitaji ulazima wa ukaguzi bali mtu mwenye nayo anaweza kupita kwenye mitambo maalum na kujulikana kuwa ni Mtanzania. Nne, Pasipoti ya Kielekitroniki inayo program maalum ambayo mwananchi anaweza kuitunza kwenye simu yake na kama Pasipoti yake ikipotea ghafla anaweza kuitumia aliyoitunza kwenye simu yake.

Mwisho Kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe. Kinawilo alitoa tahadhari kwa Watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa makini wakati wa kutoa Pasipoti za Kielekitroniki kwa wananchi ambao ni Watanzania tu na siyo kuzitoa kwa wasio raia wa Tanzania. Pia alitoa wito kwa Maafisa wa Idara ya Uhamiaji kuwasaidia wananchi watakaohitaji Pasipoti hizo na hawana uelewa wa kutumia kompyuta ili wasaidiwe kujaza fomu zao.

Katika upande mwingine Kamishina wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga alisema kuwa mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuzindua Pasipoti za Kielekitroniki Januari 31, 2018 Pasipoti hizo zilikuwa zinatolewa Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam na Zanzibar tu lakini sasa mikoa imeanzi kuzindua na kutoa Pasipoti za Kielekitroniki.

Kamishna Kihinga alisema kuwa tayari Pasipoti za Kielekitroniki zimeanza kutolewa katika mikoa ya Dadoma, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na sasa Mkoa wa Kagera ambao uzinduzi umefanyika leo Juni 8, 2018. Jumla ya Pasipoti za Kielekitroniki 17,595; zimetolewa  Pasipoti za Kielekitroniki za kawaida zikiwa 17,289 za Utumishi 56, za Kidiplomasia 248, na Diplomasia Maalum mbili tu.

Naye Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Kagera Abdalah Towo akiongea na mhadhara wa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Pasipoti za Kielekitroniki aliwakumbusha Maafisa wenzake katika Wilaya kuwa Elimu imetolewa ya kutosha kwao na ni lazima kuwaelimisha wananchi na kuwaongoza katika kupata Pasipoti za Kielekitroniki katika Wilaya zao.

 Pia Bw. Towo alitoa rai kwa wananchi waliopatiwa Pasipoti za Kielekitroniki katika uzinduzi huo kuwa mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wenzao na kuhakikisha wanapitia michakato yote wao waliyoipitia na kama kutatokea mwananchi anasema yeye hajapitia mchakato huo na amepata Pasipoti ya kielekitroniki aripotiwe mara moja katika Ofisi za Uhamiaji ili hatua zichuliwe mara moja.

Aidha, Bw. Towo alisema katika uzinduzi huo zilitolewa Pasipoti za Kielekitroniki 101 kwa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini, Wazee, Watumishi na Wananchi. Rai kwa wananchi kwa kuwa Mkoa wa Kagera umepakana na nchi tatu ni lazima wananchi kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa ili Pasipoti za Kielekitroniki zisitolewe kwa wasiokuwa raia wa Tanzania.

Kwaniaba ya Viongozi na wote waliopatiwa Pasipoti za Kielekitroniki katika uzinduzi Mkoani Kagera Baba Askofu Methodius Kilaini  Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoriki la Bukoba aliishukuru Serikali na Idara ya Uhamiaji kwa kutoa Pasipoti za Kielekitroniki kwa wananchi na alisema kuwa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera imejipanga vizuri hasa katika mapokezi ya wananchi na huduma.

“Tunashukuru sana na nimeikagua Pasipoti yangu ya Kielekitroniki na kugundua kuwa ni pasipoti nzuri sana tena  sana, sasa itatusaidia sisi kama Viongozi wa dini na wananchi katika kusafiri, naiona Tanzania ikiendana na mataifa mengine katika masuala ya mitandao.” Alisistiza Baba Askofu Kilaini

Unahitaji nini ili Upate Pasipoti ya Kielekitroniki?

Gharama ya Pasipoti ya Kielekitroniki ni Shilingi 150,000/=, Utajaza fomu hata ukiwa nyumbani ambayo inapatikana katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.Immigratino.go.tz . Viamabatanisho ni pamoja na Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa cha kwako na cha mzazi wako mmoja, Barua ya utambulisho kutoka kazini kwako/Mtendaji wa kata, Kitambulisho cha Kazi/mpiga kura, na picha tatu pasipoti size.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa