- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali Mkoani Kagera Yaweka Mikakati Thabiti ya Kufufua Zao la Pamba Wilayani Biharamulo na Muleba
Mkoa wa Kagera waweka mikakati ya kuhakikisha kuwa zao la pamba linafufuliwa upya na kupewa kipaumbele kama zao la biashara kwa wakulima na kuhakikisha kuwa zao hilo linalimwa kwa kiwango kikubwa hasa katika Halmashauri za Wilaya za Biharamulo na Muleba zilizokuwa zinalima zao hilo hapo awali.
Katika kuhakikisha zao la pamba Mkoani Kagera linafufuliwa upya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu aliwatembelea Wakaulima katika Wilaya za Biharamulo na Muleba na kuzindua ugawaji wa mbegu bora za pamba kwa wakulima Katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa ajili ya msimu huu wa mwaka 2017/2018.
Mkuu wa Mkoa Kijuu akiwa katika Wilaya ya Biharamulo Kata ya Nyamigogo Tarafa Nyarubungo na Wilayani Muleba katika Kata ya Nyakabango Tarafa ya Kimwani alikutana na wananchi na wakulima wa zao la pamba na kuwahamasisha wananchi hao kuanza tena kulipa kipaumbele zao la pamba kama zao biashara.
“Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikiksha kuwa zao la pamba linafufuliwa upya, aidha Serikali inaliangalia na kulipa kipaumbele zao la pamba kama zao mojawapo kuu la biashara ambalo kama likipewa kipaumbele na kuangaliwa kwa ukaribu litaweza kuinua pato la Taifa na wananchi kwa ujumla ambao ni wakulima wetu.” Alisistiza Mhe. Kijuu.
Mkuu wa Mkoa aliwatoa wasiwasi wananchi juu ya upatikanaji wa masoko na kusema kuwa sasa Serikali imeanzisha viwanda pia na kuhakikisha kuwa viwanda vyote vya pamba vinafufuliwa ili viweze kufanya kazi na pamba kupata soko la kutosha.” Jukumu lenu ninyi wakulima mnatakiwa kulima kwanguvu sana sasa zao la Pamba.”Alisistiza Mhe. Kijuu
Mikakati ya Mkoa kuhakikisha zao la Pamba linafufuliwa.
Mkuu wa mkoa wa Mkoa aliziagiza Halmashauri za Wilaya za Biharamulo na Muleba kuhakikisha zinawapatia mbegu bora wakulima wa zao la pamba kwa utaratibu wa kuwakopesha mbegu hizo katika msimu huu wa 2017/2018 na kuanza kujipanga vizuri zaidi kwa msimu wa mwaka 2018/2019.
Halmashauri za Wilaya za Biharamulo Muleba na kupitia Maafisa Ushirika wahakikishe wanaimarisha vikundi vya AMCOS kwa ajili ya kuviweka tayari katika kushughulikia mchakato wa kulifufua zao la pamba.
Maafisa Kilimo, Watendaji na Wataalamu waliopo wawe na mashmba darasa au mashamba ya mfano hasa katika ngazi za Vijiji na Kata. Aidha, Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji watumike kuhamasisha wakulima maeneo ambayo wataalamu wa kilimo hawapo.
Akihitimisha ziara yake aliyoifanya katika Halmashauri za Wilaya za Biharamulo na Muleba tarehe 18 hadi 19 Oktoba, 2017 Mhe. Kijuu pia aliwakumbusha wananchi na viongozi wa ngazi zote katika Mkoa kuhakikisha kila kaya inakuwa na ekari ya zao moja la biashara hususani Pamba na ekari moja ya zao la chakula kwaajili ya kujikinga na janga la njaa lakini pia wanannchi hususani wakulima kujiingizia kipato kwa zao la biashara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa