• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mtihani wa Darasa la Saba Waendelea Kufanyika Kwa Amani na Utulivu Kagera Matarajio ni Mkoa Kushika Nafasi ya Kwanza Kitaifa – RC Gaguti

Imewekwa : September 5th, 2018

Mkoa wa Kagera ukiwa mkoa mmoja wapo kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo  wanafunzi wake wa Darasa la Saba  Wavulana 22,129 na Wasichana 25,099 jumla 47,228 wanafanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi maandalizi kuanzia kuwaandaa wanafunzi, Mapokezi ya Mtihani hadi siku ya kwanza ya kufanya mtihani Septemba 5, 2018 na mtihani huo kufanyika hali ni shwari na mtihani umefanyika kama ilivyopangwa.

Kikiwa kipaumbele chake cha kwanza kuhakikisha Mkoa wa Kagera unaendelea kufanya vizuri na kushika nafasi za juu kabisa Kitaifa tangu kuripoti kwake Mkuu wa Mkoa wa Kagera BrigediaJenerali Marco E. Gaguti alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya shule katika Manispaa ya Bukoba ili kuona mitihani hiyo kama inaendelea kufanyika kama Mkoa ulivyojiandaa na kujipanga ifanyike.

Baada ya kutembelea shule za Msingi kadhaa katika Manispaa ya Bukoba ikiwemo Shule za Msingi Tumaini na Mafumbo na kuongea na wasimamizi wakuu wa vituo na Walimu Wakuu wa Shule hizo Mkuu wa Mkoa Gaguti aliridhika na maendeleo ya wanafunzi wanavyofanya mtihani pia na usimamizi unavyoendelea kuimarishwa kuhakikisha hakuna udanganyifu wowote.

“Hadi sasa hakuna changamooto yoyote katika Mkoa wetu wa Kagera ambayo nimeipokea kuhusu kufanyika kwa Mitihani ya Darasa la Saba, aidha, na mimi mwenyewe nimepita katika shule kadhaa kuona namna zoezi hili linavyoendelea, naona wahusika wote pamoja na wanafunzi wanaendelea na majukumu yao bila wasiwasi.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Pia Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwa watendaji wote waliokabidhiwa jukumu la kusimamia Mitihani ya Darasa la Saba kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa kusimamia Mitihani hiyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu hadi mitihani itakapokamilika na kukabidhiwa mahali panapohusika bila kujihusisha na vitendo vyovyote vya hujuma vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Ufaulu wa Mitihani ya Darasa la Saba Mkoa wa Kagera: Kwa ujumla Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa Mikoa inayofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba. Mwaka 2017 ulishika nafasi 3 kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara ikilinganishwa na nafasi ya 5 mwaka 2016 kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara pia ikilinganishwa na nafasi ya 7 mwaka 2015 kati ya Mikoa 25 na nafasi ya 8 mwaka 2014 kati ya Mikoa 25.

Mkuu wa Mkoa Gaguti amewatakia heri na ufaulu mzuri wanafunzi wote wanaofanya Mtihani wa Darasa la Saba Mkoani Kagera na kusema kuwa imani yake mwaka huu Mkoa wa Kagera utongoza Kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa.  Jumla ya Shule 953 Katika Mkoa wa Kagera 890 zikiwa za Serikali na 63 Binafsi zenye watahiniwa jumla 47,228 zinafanya Mtihani wa Darasa la Saba.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa