• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

MV Victoria Kurudi Kidigitali Meli Mpya Tayari Imeanza Kujengwa Wananchi Kagera Jipangeni Kuelekea Uchumi wa Kati

Imewekwa : October 24th, 2019

Wakati Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli inaendelea kujenga miradi mikubwa ya kimkakati ya kuelekea katika uchumi wa kati bado Mkoa wa Kagera haujasaulika bali sasa wananchi wake wanakumbushwa kujiandaa kikamilifu kwa kuchapa kazi za kilimo na biashara wakati nchi inaelekea katika mapinduzi makubwa ya kiuchumi ili kutembea na kasi ya uchumi wa kati.

Ni baada ya meli ya MV Victoria meli kongwe na maarufu kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera  kukamilika ukarabati wake ifikapo Machi 2020 na kurejea katika Ziwa Victoria kwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Bukoba na Kemondo  kusafirisha abiria zaidi 1000 pamoja na mizigotani 200 ambapo kutakuwepo na nafuu kubwa ya bidhaa za viwandani pamoja na usafiri wa wananchi kati ya Bukoba na mwanza.

Uhakika wa meli ya MV Victoria kukamilika ukarabati wake mwakani Machi 2020 pia na ujenzi wa meli mpya ulishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti pamoja na Kamati ya amani ya Mkoa wa Kagera iliyowajumuisha viongozi wa dini watatu Askofu Methodius Kilaini Askofu msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Dk. Abednego Keshomshahara  Askofu wa (KKKT) Jimbo la Kasikazini Magharibi na Sheikh Haruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa Gaguti akiwa katika ziara hiyo ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ukarabati  na ujenzi wa Meli mpya pamoja na cherezo katika Bandari ya Mwanza Kusini alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli  kwa kuleta mradi huo kwa ajili ya ukombozi wa kiuchumi  wa wananchi wa Kagera kwani utaweka usafiri wa uhakika pia alitoa wito kwa wananchi wa Kagera kujielekeza katika kazi zenye tija za kilimo na biashara na kujiandaa kutumia maboresho ya usafiri kuinua uchumi wa mkoa.

Askofu Msaidizi Methodius Kilaini baada ya kuiona miradi hiyo mitatu alisema kuwa anamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza maajabu katika miradi ya ujenzi na ukarabati wa meli, aidha alisema kuwa Mkuu wa Mkoa Gaguti amewafanyia jambo jema sana la kuwafanya wao kama viongozi wa dini wapate nguvu ya kuleta tumaini na uelekeo kwa watu na kuufanya Mkoa wa Kagera kusimama tena kiuchumi.

Askofu Dk. Keshomshahara mara baada ya kujionea ujenzi wa meli mpya na cherezo na ukarabati wa Meli ya MV Victoria alisema kuwa sasa wao kama viongozi wa dini wamepata neno la kuwaeleza waamini wao na kuwahamasisha kujiandaa kwaajili ya kuitumia fursa ya Meli hizo zikikamilika . Sheikh Haruna Kichwabuta naye alisema kuwa Rais Magufuli alihaidi wakati wa kampeini sasa ametekeleza bila ahadi hewa hasa kwa wananachi wa Mkoa wa Kagera.

Bw. Eric B. Hamissi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli nchini alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti kutembelea miradi hiyo ya ujenzi na ukarabati wa meli na kutoa wito kwa wananchi na viongozi wengine nchini kwenda kutembelea miradi hiyokujionea maendeleo ya ujenzi wa meli mpya na cherezo pia na ukarabati wa meli za zamani.

Bw. Eric alisema kuwa mradi  unatekelezwa na Kampuni ya JV of Gas Entec  CO. Ltd  Kang Nam Corporation na SUMA JKT  ambapo kwa ujumla utagharimu jumla ya shilingi bilioni 152 na tayari Serikali imetoa shilingi bilioni 60 wakandarasi wanadaiwa kazi hawaidai Serikali aidha, mradi umegawanyika  katika sehemu kuu nne. Kwanza ni ujenzi wa meli mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 400 Abiria 1200 ikiwa na urefu wa meta 92.6, urefu kwenda juu meta 11.2 (sawa na ghorofa nne) na upana wa meta 17 na gharama yake ni shilingi bilioni 90.

Mradi wa pili ni ujenzi wa cherezo ambacho kitakuwa na uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa tani 4000 ambapo meli mpya itakuwa na uzito wa tani 3500 tu aidha, cherezo kama  hicho hakuna katika nchi za Afrika Mashariki na Kati  na kikikamilika kitaiingizia Serikali Mapato kama kitatumika kwa kujenga meli zenye uzito mkubwa hasa kutoka nje ya Tanzania.  Mradi wa cherezo utagharimu shilingi bilioni 36 na ujenzi wake umefikia asilimia 52.

Mradi wa tatu ni ukarabati wa Meli ya MV Victoria ambao utagharimu shilingi bilioni 22.8 na ukarabati wa meli hiyo umefikia asilimia 50 ambapo inakarabatiwa ikiwa ni pamoja na kubadilishwa mfumo wake wa zamani na kuwekewa mfumo wa kidigitali. Mradi wa wa nne ni ukarabati wa meli ya Butihama ambapo mradi huo nao utagharimu shilingi bilioni 4.9 na ukarabati wake umefikia asilimia 40.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa