- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wadau Mkoani Kagera Wamuunga Mkono Mkuu wa Mkoa Upatikanaji wa Damu Katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukusanyaji wa Damu
Wadau mbalimbali katika Mkoa wa Kagera wamuunga mkono Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Katika kuadhimisha wiki ya kilele cha ukusanyaji wa damu kuanzia tarehe 11 hadi 15 Desemba 2017 kwa kuchangia bidhaa mbalimbali kama maji, soda, bisukuti na ‘Ream’ za Karatasi ili kusaidia kukusanya damu kwaajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.
Akitoa maelezo wakati Wadau hao wakikabidhi bidhaa hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Desemba 13, 2017 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. John Mwombeki alisema kwa siku nne kuanzia tarehe 11 hadi 15.12.2017 ulifanikiwa kukusanya ‘unit’ 900 za damu kwa kila Wilaya kukusanya ‘unit’ 100.
Aidha, Dk. Mwombeki alisema kuwa kutokana na umuhimu wa damu katika hospitali na maisha ya wananchi kupitia Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu waliwaomba wadau mbalimbali kuchangia bidhaa kama maji, soda, na bisukuti ambavyo hutolewa kwa mwananchi ambaye hufika katika kituo kujitolea damu.
“Mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na watu milioni 2.5 na kutokana takwimu za kisayansi mahitaji ya damu unatakiwa kuwa na asilimia 1% hadi asilimia 2% za damu kwa wananchi waliopo katika eneo lako kwa mana hiyo Mkoa wa Kagera unatakiwa kuwa na kiasi cha damu ‘unit’ 25,000 kwa mwaka kuweza kuwafikia wahitaji wa damu kama akina mama wajawazito, wananchi mbalimbali wanaopta ajali,” alifafanua Dk. Mwombeki.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu akiwashukuru Wadau alisema amefurahishwa sana na kitendo chao cha kuitikia wito wake wakusaidia upatikanaji wa damu katika mkoa wa Kagera ili kuokoa maisha ya wananchi wanaotakiwa kupata huduma ya damu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma kwenye mkoa.
Mhe.Kijuu alitoa wito kwa wananchi kuendelea kufika katika vituo vya kutolea damu ili kujitolea damu na alisistiza kuwa kutoa damu kuna nyingi kwanza mwananchi anayetoa damu anapatiwa kadi ambapo anakuwa mwanancha na siku akipata tatizo la kiafya akahitaji damu anasaidiwa haraka sana kwasababu ni mwanachama.
Vilevile Mhe. Kijuu alitoa wito kwa wananchi kujitolea damu ambapo alisema kuwa hiyo ni fursa mojawapo ya mwananchi kuijua afya yake kupitia kujitolea damuambapo damu hiyo hupimwa na mwananchi huyo kupewa majibu na kumfanya kujilinda na magonjwa mbalimbali kama UKIMWI, Kisukari na mengineyo.
Wadau waliotoa bidhaa ni pamoja na Kampuni ya TANICA katoni 50 za maji, Benki ya CRDB walitoa katoni 20 za maji, Benki ya NMB walitoa ‘ream’ karatasi za limu katoni nne kwaajili ya kuchukulia takwimu za wananchi wanaofika kutoa damu , bisukuti katoni 5, soda katoni 25 na maji katoni 25
Maadhimisho ya kilele cha ukusanyaji damu huadhimishwa kitaifa kila mwaka wiki moja kabla ya Siku Kuu za mwisho wa mwaka. Mwaka 2016 mkoa wa Kagera uliweza kukusanya kiasi cha ‘unit’ 7,000 tu badala ya ‘unit’ 25,000, wito kwa wananchi ni kujitolea kutoa damu ili kuokoa maisha ya wahitaji ili angalau kwa mwaka huu 2017 mkoa uweze kufikia nusu ya mahitaji kuokoa maisha ya wananchi wengi zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa