- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenge wa Uhuru ukiendelea na mbia zake na kukimbizwa Mkoani Kagera tayari umetembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ipatayo 39 yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 15,099,837,309 kati ya miardi 74 ya mkoa mzima yenye thamani ya shilingi bilioni 18,894,323,585.90
Tangu kupokelewa kutoka Mkoa wa Kigoma Aprili 24, 2019 Mwenge wa Uhuru 2019 tayari umekimbizwa katika Wilaya tano za Ngara, Karagwe, Kyerwa Missenyi na Bukoba ambapo katika Wilaya ya Bukoba umekimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba leo Aprili 28, 2019.
Katika kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatakiwa kutoa huduma kwa wananchi au tayari inatoa huduma hizo, Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 kupitia Kiongozi wake Mzee Mkongea Ali pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wenzake wamekuwa wakikagua miradi kwa umakini mkubwa kuhakikisha kuwa taratibu, kanuni na sheria pia viwango vya miradi hiyo kama vilizingatiwa wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Sambamba na ukaguzi huo pia Wakimbiza Mwenge Kitaifa wamekuwa wakikagua nyaraka mbalimbali za utekelezaji wa miradi na kuagiza kila nyaraka ya mradi mfano mikataba na ramani kuwepo katika eneo husika la mradi jambo ambalo halikuzingatiwa ipasavyo na baadhi ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Ngara na Manispaa ya Bukoba na kupelekea jumla ya miradi mitano katika Halmashauri hizo kutokuzinduliwa au kuwekewa mawe ya msingi.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara miradi miwili ya (ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, bwalo, bweni na maktaba shule ya Sekondari Murusagamba) na mradi wa maji Rulenge yenye jumla ya thamani ya shilingi 942,659,018 haikuwekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali kutokana na kukosekana kwa baadhi ya nyaraka muhimu za utekelezaji wa miradi hiyo.
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba jumla ya miradi mitatu kati ya kumi (Mradi wa Jengo la viwanda vidogo SIDO Rwamishenye, Mradi wa Maji Makongo Bushwa na Mradi wa Shule ya Msingi Tumaini) yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 2,050,071,701 haikuzinduliwa kutokana na kukosa baadhi ya nyaraka muhimu wakati wa utekelezaji wake.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake Mkoani Kagera katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Aprili 29, 2019 Halmashauri ya Wilaya Muleba Aprili 30, 2019 na utahitimisha mbio zake Wilayani Biharamuo Mei Mosi, 2019 na kukabidhiwa Mkoani Geita Mei 2, 2019.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa