- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika hafla fupi iliyofanyiaka katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Agosti 6, 2018. Aidha, mara baada ya kukabidhiwa ofisi Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti alimwapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashidi Mohamed Mwaimu.
Mara baada ya kukabidhiwa Rasmi Ofisi Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ambaye sasa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa 23 tangu uhuru mwaka 1961 alimshukuru mtangulizi wake Mhe. Kijuu na kuhaidi kutomwangusha kwa juhudi zake alizozifanya katika kuleta maendeleo ya Mkoa wa Kagera.
“Nihaidi wananchi wa Mkoa wa Kagera Utumishi uliotukuka pia nikuhaidi Mzee wangu Mhe. Kijuu kuwa nikiwa hapa Mkoani Kagera kama Mkuu wa Mkoa nitahakikisha naendeleza juhudi zako zote ulizokuwa ukizifanya kuwaletea maendeleo wananchi wa hapa Kagera, kikubwa nitaomba ushirikiano mkubwa kutoka kwao,” Alifafanua Mhe. Gaguti.
Mambo Muhimu ambayo Mhe. Gaguti amehaidi kuyafanyia kazi yeye kama Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera ni Kudumisha Ulinzi na Usalama wa Mkoa hasa katika mipaka na nchi jirani kwa kudhibiti magendo ya mazao hasa kahawa, kudhibiti uingizwaji wa mifugo katika Misitu ya Akiba na Hifadhi ambayo sasa Serikali imeyatangaza kuwa hifadhi za Taifa.
Pia Mhe. Gaguti alisema atahakikisha kuwa fursa ya kuwa na mipaka na nchi jirani inatumika ipasavyo ili kuinua uchumi wa Mkoa wa Kagera kwa wananchi kufanya biashara na nchi jirani ili kujiongezea kipato na kunufaika na mipaka ya nchi zinauzunguka Mkoa wa Kagera.
Naye Mkuu wa Mkoa aliyemaliza muda wake Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu mara baada ya kukabidhi ofisi rasmi akitoa neno la kuwaaga wananchi wa Kagera alisema kuwa anamshukura Rais John. Pombe Magufuli kwa kumkubalia kustaafu ili akapumzike. Aidha, aliushukuru uongozi wa mkoa pamaoja na wananchi wa Kagera kwa ushirikiano waliompatia wakati akitekeleza majukumu yake na kuwaomba pia ushirikiano huo waendelee kumpatia Mhe. Gaguti.
Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Askofu Msaidi wa Jimbo Katoriki la Bukoba Methodius Kilaini wakimuaga Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe. Kijuu walimtakia maisha mema katika mapumziko yake, aidha, walimshukuru kwa kuuvusha Mkoa wa Kagera katika kipindi kigumu hasa wakati wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016.
Naye Mkuu wa Wilya ya Kyerwa Rashidi M. Mwaimu mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti alisema kuwa kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa ananshirikiana na watendaji mbalimbali katika Wilaya ya Kyerwa kukuza na kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mstaafu Kanali Mstaafu Shabani Lissu akiwaaga wananchi wa Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Kyerwa alisema anamshukuru Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kumteua na kutumikia wananchi wa Wilaya ya Kyerwa kwa miaka miwili akiwa Mkuu wa Wilaya hiyo.
Aidha, Kanali Mstaafu Shabani Lissu alisema kuwa amefikisha muda wake wa kustaafu kwa umri kwani amefikisha miaka 61 na alilitumika Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa miaka 36 na miaka miwili alitumika kama Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa na sasa amestaafu kwenda kupumzika katika majukumu ya Kiserikali.
Wananchi wa Mkoa wa Kagera tunakukaribisha Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashidi Mohamed Mwaimu kuja Kagera na Kyerwa kuchapa kazi kuwaletea wananchi wetu maendeleo. Kagera tunayo kaulimbiu yetu isemayo “Kagera, Kazi Amani na Maendeleo” karibuni tuidumishe kaulimbiu hiyo kwa vitendo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa