• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Natamani Kuona Mwalimu wa Kagera Anastaafu Akiwa Tajiri Benki Kuna Fedha Zinasubiri Maandiko Yenu ya Miradi – RC Gaguti

Imewekwa : September 24th, 2019

Kama kuna mtumishi yeyote awe hapa au nje ya hapa tena ambaye ni mwalimu hajishughulishi kukopa kwenye taasisi za kifedha huyo anaishi tu hawezi kupata maendeleo kamwe bali atabakia kubadili mboga kila siku na kuvaa suti au kubadilisha mavazi mpaka anastaafu katika utumishi wake wa uma.

Maneno hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti  Septemba 23, 2019 wakati akifungua kongamano la Walimu na Benki ya NMB Bukoba katika siku ya walimu kwenye ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba .

Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaeleza walimu hao ambao ni wadau wakuu wa Benki ya NMB kuwa wanayo kila haki ya kufurahia maisha yao kwani Serikali inawajali lakini pia Benki ya NMB imeboresha maisha yao kupitia mikopo ambayo inawafanya wafanye kazi zao kwa uhakika na umairi mkubwa.

Mhe. Gaguti alisema kuwa mkoa wa Kagera umekuwa ukifanya vizuri katika mitihani mbalimbali ya kitaifa lakini sababu kubwa ni kuwa walimu wanafanya kazi yao kwa kuridhika ikiwa ni pamoja na Serikali kuwajali kwa kuwalipa mishahara na stahiki zao lakini pia Benki ya NMB imewafanya waboreshe maisha yao kwa mikopo.

“Nikiwaangalia hapa naziona nyuso za matumaini zenye bashasha na furaha  lakini niwaeleze ukweli ni kwamba hata mimi baba na mama walikuwa walimu na tayari wamestaafu, kwa maisha ya sasa ya fursa zilizopo walimu waliostaafu wanatamani sana kurudi kazini kwani zamani fursa hizi za sasa  hazikuwepo na sababu nyingine ni Benki ya NMB nayo imechangia sana kuboresha maisha yao”. Alisisitiza Mhe. Gaguti.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alito rai kwa benki ya NMB kuona namna ya kuwapunguzia riba walimu sababu ni wadau wakubwa wa benki hiyo tangu mwanzo. Pia aiwataka walimu kutanua wigo wa kuunda vikundi vya pamoja mafano kwenye Kata na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato vyao hasa pale wanapostaafu. 

Naye Bw. Omari Mtiga Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi akieleza dhumuni la kukutana na walimu hao  alisema kuwa ni kuwaelimisha juu ya huduma zao mpya ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni yao juu ya huduma za Benki ya NMB wakiwa kama wadau wakubwa wa benki hiyo. Aidha, Bw. Mtiga alisema kuwa walimu wameanzia mbali na Benki ya NMB enzi za kufanya kazi kwa makaratsi hadi sasa enzi za digitali bado ni wateja wao wakubwa.

Mwalimu Thomas Ngirwa Mkuu wa shule ya Sekondari Bukara kwaniaba ya walimu wenzake alisema kuwa Benki ya NMB ni mkombozi kwa walimu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kwani alisema kuwa shule yake ya Bukara imewahi kupata msaada wa madawati sitini kwa ajili ya wanafunzi ikiwa naye binafsi amekuwa akikopa fedha kutoka NMB kwaajili ya kusomesha watoto wake.

Mwisho, Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwa walimu hao kuwa mabalozi wazuri wa kulipa kodi kwa kuwa mkoa wa Kagera bado haufanyi vizuri katika kodi ambazo zinajenga miradi ya maendeleo kwa wananchi. “Popote mtakaposimama au kupata nafasi toeni elimu kwa kila mwananchi kununua bidhaa adai risiti na kuwahamasisha wanaouza kutoa risisti, walimu mna nguvu kubwa katika jamii”. Alihitimisha Mhe. Gaguti

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa