• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Ni Lazima Zaidi ya Wanafunzi Elfu Kumi na Nne Waliofaulu na Kukosa Vyumba Vya Madarasa Waanze Masomo Yao Pamoja na Wenzao Ifikapo Januari 7, 2019 – RC Kagera

Imewekwa : December 19th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti awaongoza Wadau wa Elimu Mkoani Kagera kuweka mikakati ya muda mfupi na mda mrefu ili kuhakikisha wanafunzi 14,046 kati ya wanafunzi 39,545 waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2018 na kukosa Vyumba vya Madarasa wanaanza masomo yao kama wenzao 25,499 ifikapo Januari 7, 2019.

Mikakati hiyo iliwekwa katika kikao cha Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Kagera kilichofanyika Mkoani hapa Desemba 18, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Bukoba na kuongozwa na Mhe. Gaguti ambapo baada ya majadiliano ya muda mrefu katika kikao hicho wadau walikubaliana kuwa na mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili kuokoa jahazi la wanafunzi 14,046 ambao wamefaulu kuingia kidato cha kwanza na wangekosa vyumba vya madarasa shule zinapofunguliwa Januari 7, 2018.

Mikakati ya muda mfupi ni pamoja na Shule ambazo zipo maeneno ya mijini ambapo wanafunzi hawatoki mbali na shule hizo uwekwe utaratibu wa ufundishaji kwa awamu mbili, awamu ya kwanza asubuhi na awamu ya pi mchana wakati vyumba vya madarasa vikiendelea kukamilishwa. Pili, Mamlaka za Serikali za Mitaa zihakikishe zinakamilisha vyumba 351 pamoja na samani zake ifikapo Januari 7, 2019 wanafunzi wote waliofaulu waweze kuingia madarasani.

Mkakati mfupi wa tatu ni Fedha za mifuko ya Majimbo zielekezwe katika ujenzi wa madarasa ili kukamilisha haraka ujenzi wa miundombinu hiyo na kuruhusu wanafunzi 14,046 kuingia madarasani. Aidha, mipango ya muda mrefu ni pamoja na Mkoa kupadisha asilimia ya kiwango cha ufaulu cha sasa cha asilimia 84.42% hadi asilimia 95% ifikapo Desemba 2019.

Pili, Mipango ya Halmashauri za Wilaya izingatie uhalisia wa takwimu ili kuweka maoteo sahihi ya miundombinu ya elimu.Tatu, Mkoa wa Kagera kupunguza mimba za utotoni kwa asilimia 50% ifikapo Desemba 2019. Mwisho Kikao cha Wadau kifanyike mwezi Machi 2019 kujadili namna ya kutatua changamoto za Elimu Mkoani Kagera na kuona mikakati iliyowekwa ya muda mfupi kama imetekelezeka.

Matokeo ya Wanafunzi wanaotarajiwa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2019

Mwaka 2018 Mkoa wa Kagera ulikuwa na jumla ya watahiniwa 47,197 waliotarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi.  Kati ya hao wavulana walikuwa 22,124 na wasichana 25,073.  Watahiniwa waliohitimu ni 46,795 sawa na asilimia 99.11 ya wanafunzi waliotarajiwa. Vile vile kuna jumla ya Wanafunzi 86 wenye mahitaji maalum, kati yao wavulana ni 50   na wasichana ni 36.

Watahiniwa  waliofaulu ni 39,545 sawa na asilimia  84.42 ya watahiniwa waliofanya mtihani, ambapo miongoni mwao ni wavulana ni 18,553 na wasichana ni 20,992. Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 0.02 ukilinganisha na kiwango cha ufaulu cha asilimia 84.4. kwa mwaka 2017. Kiwango cha ufaulu  kilichokuwa kipangwa katika mkoa kilikuwa ni 88%.

Jumla ya wanafunzi 25,499  ambapo miongoni mwao  wavulana 12,356 na wasichana 13,143  sawa na asilimia 64.48, ndio waliopata nafasi ya kujinga kidato cha kwanza kwa awamu hii ya kwanza kwa kuzingatia vyumba vya madarasa vilivyopo. Aidha wanafunzi 14,046 wakiwemo wavulana 6,257 na wasichana 7,789 sawa na 35.52% wamefaulu lakini kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa wanasubiri ujenzi wa vyumba vya madarasa kukamilika.

Mahitaji ya Miundombinu katika Shule za Sekondari

Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 791, vilivyopo ni 546, Upungufu ni vyumba 245 sawa na asilimia 30.96%. Vyumba hivyo vilivyopo vya madarasa vitachukua wanafunzi wa kidato cha kwanza 25,499 wavulana wakiwa 12,356 Wasichana 13,143 sawa na asilimia 64.5. Vyumba vya Maabara katika Shule za Sekondari Mahitaji ni 570 vilivyopo 218 upungufu 352 sawa na asilimia 61.75 (Taarifa nyingi za kitakwimu Tembelea Tovuti ya Mkoa wa Kagera www.kagera.go.tz)

Pamoja na Mkoa wa Kagera kuweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba  wanakwenda Shule za Sekondari mwaka 2019 lakini Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti aliwapongeza wadau wote wa Elimu pamoja na wananchi wote wa Kagera kwa kutambua umuhimu wa elimu na kuufanya Mkoa kushika nafasi za juu katika ufaulu kwenye mitihani mbalimbali ya Kitaifa.

“Nawapongeza sana wote mliopo hapa pia na wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kwa kutambua umuhimu wa Elimu kwani Mtihani wa Darasa la Saba mwaka huu 2018 Mkoa umeshika nafasi ya 5 kati ya Mikoa 26, Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2017 Mkoa ulishika nafasi ya 9 kati ya Mikoa 26, Matokeo ya Kidato cha Sita Mkoa ulishika nafasi ya 5 kati ya Mikoa 26, na Mkoa wa Kagera umeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfurulizo katika Matokeo ya Darasa la Nne.” Alitoa Shukrani Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Mhe. Gaguti alimalizia kwa kuwataka Wadau wa Elimu na wananchi wote katika Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanashirikiana  na kuendelea kuinua zaidi kiwango cha elimu kufikia asilimia 95% kutoka asilimia ya sasa 84.42% pia Mkoa wa Kagera kuongoza kwa kushika nafasi za kwanza katika mitihani yote ya Kitaifa.

Ufaulu katika Mkoa wa Kagera ngazi ya Halmashauri, Halimashauri ya Wilaya ya Biharamulo imekuwa ya 1 kimkoa (Kitaifa ya 11) mwaka huu 2018, mwaka 2017 ilikuwa ya 2 Kimkoa (Kitaifa ya 19). Bukoba Manispaa imekuwa ya 2 Kimkoa na 20 Kitaifa na mwaka 2017 ilikuwa ya 1 Kimkoa na ya 12 Kitaifa. Ngara imekuwa ya 3 Kimkoa na ya 30 Kitaifa mwaka 2017 ilikuwa ya 8 Kimkoa na ya 52 Kitaifa. Muleba imekuwa ya 4 Kimkoa nay a 38 Kitaifa  na Mwaka 2017 ilikuwa ya 3 Kimkoa na Kitaifa ya 23.

Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imekuwa ya 5 Kimkoa na Kitaifa ya 48 na mwaka 2017 ilikuwa ya 5 Kimkoa na  ya 35 Kitaifa. Bukoba Vijijini imekuwa ya 6 Kimkoa na ya 66 Kitaifa na mwaka 2017 ilikuwa 4 na ya 25 Kitaifa. Kyerwa imekuwa ya 7 Kimkoa na ya 91 Kitaifa na mwaka 2017 ilikuwa ya 7 Kimkoa na ya 49 Kitafa. Karagwe imekuwa ya mwisho ya 8 Kimkoa na ya 96 Kitaifa na mwaka 2017 ilikuwa ya 6 Kimkoa na ya 36 Kitaifa ambapo Karagwe ilikabidhiwa kinyago na Mkuu wa Mkoa kwa kushika nafasi ya mwisho Kimkoa.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa