- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Operesheni ya Kunusuru Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba Kagera Yanasa Mifugo 3053 na Kuwatia Hatiani Watuhumiwa Watano
Operesheni ya kuondoa wavamizi na waharibifu wa Mapori ya Akiba, Hifadhi za Misitu, Mapori Tengefu na Maeneo ya vyanzo vya maji Mkoani Kagera tayari imekamata jumla ya mifugo 3,053 na kukuwakamata watuhumiwa 19 ambao tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo April 3, 2017
Operationi ya kunusuru Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba Mkoani Kagera imeanza rasmi Machi 30, 2017 mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoa muda wa siku tatu kuanzia Machi 18-21, 2017 kwa wavamizi wote kuondoka na kuondoa mifugo yao kwa hiari katika hifadhi hizo.
Mara baada ya muda wa kuondoka na kuondoa kwa hiari mifugo kuisha na operesheni kuanza, Mifugo iliyokamatwa kwenye Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba Mkoani Kagera ni Pamoja na Ng’ombe 2905, Mbuzi 113, na Kondoo 35 ambapo kazi inaendelea kufanyika kuhakikisha hakuna mvamizi yeyote atakayebaki katika Hifadhi hizo.
Hatua Zilizochukuliwa
Watuhumiwa 19 tayari wamekamatwa na kufikishwa Makamani kwa makosa mbalimbali ya kuendesha shughuli za kibinadamu katika Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba ambapo akitoa ufafanuzi mara baada ya kutoka Mahakamani Wakili wa Serikali Mwandamizi Athumani Matuma Kirati akiambatana na Mawakili wenzake wawili wa Serikali Erastus Anosisye na Haruna Shomari alisema;
“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufikia April 2, 2017 ilikuwa imepokea mafaili 12 yanayohusiana na makosa mbalimbali katika Hifadhi za Wanyamapori na Hifadhi za Misitu ambapo watuhumiwa 19 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa makosa ya kuingia bila kibali katika hifadhi, kuchunga mifugo katika hifadhi za Misitu na Wanyamapori, kukutwa na mazao ya Misitu bila kibali na kukutwa na zana za kuvunia mazao ya misitu kama misumeno na shoka.” Alifafanua Wakili Matuma.
Makosa mengine ni kukutwa na vifaa vya kusafirishia mazao ya misitu kama baiskeli, na kuvuna mazao ya misitu (Kambapori) bila kibali au idhini ya mamlaka husika. Katika kesi hizo 12 zilizofikishwa mahakamani kesi tatu tofauti zilimalizika kwa watuhumiwa watano kukiri makosa yao na kutozwa faini ya shilingi 100,000/= (laki moja) hadi shilingi 500,000/= (laki tano) au kifungo cha mwaka mmoja kwa kila kosa.
Pia Wakili Mwandamizi Matuma alisema ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali inaendelea kupokea mafaili mengine ya kesi na mara baada ya kuyapitia na kukaridhika na vielelezo vya ushahidi watawasilisha kesi hizo Mahakamani. Kesi tatu zilizokamilika na kutolewa hukumu na Mahakama ni Kesi namba 83, 85, 79 za mwaka 2017 ambapo jumla ya watuhumiwa watano walikiri makosa yao na kuhukumiwa kamailivyotajwa hapo juu.
Kuhusu mifugo iliyokamatwa Wakili Mwandamizi wa Serikali Bw. Matuma alisema kuwa Mahakama itatoa uamuzi mara baada ya kutembelea maeneo ya mifugo ilikokamatiwa na kuhifadhiwa katika hifadhi ili kujionea na kukubali kiwe kielelezo cha ushahidi. Kesi zote 12 ziliskilizwa na tatu kutolewa uamuzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo Niku Mwakatobe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa