• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Profesa Ndalichako Azindua Chuo Cha VETA Ndolage Aagiza Uongozi wa VETA Kukamilisha Miundombinu ya Chuo Hicho Kwa Gharama Zao Wenyewe

Imewekwa : November 27th, 2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako azindua rasmi Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Ndolage Wilayani Muleba pamoja na kutoridhishwa na matumizi ya shilingi milioni 281,575,270.6 zilizotumika kukamilisha  vyumba vya madarasa  vinne ambavyo vilikuwa vimefikia hatua ya renta na ujenzi wake ulianzishwa na wananchi wa Kijiji Bushagara.

Profesa Ndalichako akihutubia wananchi wa Kijiji cha Bushagara Kata Kamachumu chuoni Ndolage alisema pamoja na kuzindua chuo hicho lakini wananchi  wa eneo hilo hawakustahili kupata majengo aliyoyazindua bali walistahili kupata kilicho bora zaidi ya pale na kumwagiza Bw. Peter Maziku Maduki, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuchukua hatua kwa watendaji wa VETA ambao wanatekeleza miradi chini ya kiwango huku matumizi ya fedha yakiwa hayaridhishi.

"VETA mliomba wenyewe fedha shilingi milioni 281,575,270.6 na changamoto nilizozisikia mnazitaja hapa siyo changamoto kwangu kwani fedha mliomba wenyewe na mlijua kuwa mahitaji hayo mliyoyataja kama changamoto kabla ya chuo kuanza lazima yakamilike na chuo ndipo kianze. Naagiza kwenye bajeti yenu ya VETA ya mwaka 2019/2020 kata posho zote na kufikia Mwezi Juni 2020 muwe mmekamilisha majengo yote yanaohitajika katika chuo hiki." Aliagiza Profesa Ndalichako.

Taarifa ya ujenzi wa chuo cha VETA Ndolage iliyosomwa na  Bw. Buruhi Mitinje Mkuu wa Chuo cha VETA Kagera aliyehusika kusimamia ukamilishwaji wa majengo ya Chuo cha VETA Ndolage ilibainisha kuwa zilitumika shilingi 177,565,000 katika ujenzi wa majengo.

Samani na vifaa vya kufundishia viligharimu         shilingi 70,122,750 kuunganisha umeme shilingi 12,201,162.24 na gharama za Ramani (QS) na ulinzi shilingi 380,00  jumla shilingi 260,268,912.24 aidha, shilingi 21,600,000  zilitengwa kwaajili ya kuendeshea mafunzo.

Profesa Ndalichako alisema kuwa haiwezekani vyumba vinne vilivyokuwa vimefika hatua ya renta vikamilishwe kwa shilingi milioni 16 kila kimoja, jengo la utawal ambalo ni dogo sana haliwezi kugharimu shilingi milioni 42 pia karakana isiyokuwa na milango na madirisha gharama yake haiwezi kuwa shilingi milioni 21 na kiasi cha shilingi milioni 36 kutumika kuvuta umeme na kuweka miundombinu ya umeme katika majengo hayo.

“Haiwezekani sisi tunajenga chumba cha darasa kimoja kwa gharama ya shilingi milioni 20 katika mradi wa lipa kulingana na matokeo ambapo chumba hicho kinawekewa hadi vigae madirisha ya kisasa ya aluminium lakini hapa mlikuta vyumba vinne vimefikia hatua ya renta alafu kila chumba kigharimu shilingi milioni 16 haiwezekani.” Alisistiza Profesa Ndalichako  

Katika hatua nyingine Mbunge wa Muleba Kasikazini Charles Mwijage aliuomba uongozi wa VETA kuhakikisha wanaendesha mafunzo ya fani ambazo zitalenga vijana na wananchi wa eneo la Ndolage kujiajili ambapo fani hizo alizitaja ikiwemo namna ya kusindika ndizi, upambaji, usindikaji wa nyanya pamoja na maparachichi.

Chuo cha VETA Ndolage kitafunguliwa na kuanza kutoa mafunzo rasmi mwakani 2020 na kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wa mafunzo ya muda mrefu 80 na wanafunzi wa kozi fupi fupi 300 katika fani mbalimbali kwa mwaka.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa