- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa, Mhe. Fatma Mwassa amewashukuru wana Kagera kwa mapokezi mazuri huku akiomba kwa pamoja kuungana na kushirikiana ili nafasi yake ya uongozi iwe na maana halisi.
Akizungumza na viongozi mbalimbali na watumishi katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais analeta fedha nyingi Kagera na anataka kuona mipango ile anayoiletea fedha inatekelezwa na kuleta matokeo.
“Mimi jukumu langu ninapopewa kijiti ni kuja kuyaendeleza yale ambayo mmeyaanzisha, sijaja kutunga jambo jipya bali kuungana na nyinyi kuyaendeleza yale mliyo yapanga ili kuyafanya yatokee na ikiwezekana yatokee kwa haraka zaidi,” ameeleza Mhe Mwassa
Sambamba na hayo amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kumteua tena kuwa Mkuu wa Mkoa na kumpangia kituo cha Kagera. Kwani ni nafasi adhimu ambayo amempa kuja kuungana na wana Kagera kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wake Mhe Albert Chalamila amshukuru sana Mungu kwa kuondoka Kagera akiwa na utambuzi. Na kuongeza kuwa wamekuja kwenye vituo vipya kwa matakwa ya Mheshimiwa Rais ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani yake kubwa juu yao kati yake na Mhe. Fatma Mwassa. Imani ya Mheshimiwa Rais kwao ni kubwa na lazima waendelee kuitumikia kama ambavyo yeye Rais amewaamini.
Aidha ameeleza kuwa kuondoka katika majukumu yaleyale pongezi zinakuwa nyingi lakini wewe yuleyule ukiondoka kwa kushushwa cheo maneno pia uwa ni mengi. Hivyo amemsihi Mhe. Fatma kutokuogopa kutekeleza majukumu ya msingi kwasababu kila jambo uwa halikosi jawabu.
Pia ameeleza kuwa viongozi wote wapo kwaajili ya kutekeleza maono ya Mheshimiwa Rais kwasababu uongozi ni uwezo wa kufafanua maono hivyo sisi tupo kwa ajili ya kufafanua maono ya Rais na maono ya Nchi
Katika kufafanua maono tunahitaji kuendeleza mshikamano na Umoja kwasababu katika umoja ndio tunaweza tukatafsiri maono ambayo Mheshimiwa Rais ameyaweka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa