- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amaliza mgogoro wa wakulima na wafugaji uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi na moja katika Kijiji cha Kahundwe kata Chanika Tarafa Kituntu Wilayani Karagwe ni baada ya kukutana nwa wananchi wa kijiji hicho na kutoa msimao wa Serikali na kuonya juu ya uvunjifu wa amani uliowahi kutokana na mgogoro huo mwaka 2008.
Awali kabla ya kwenda Kijijini Kahundwe Februari 26, 2019 kuwasikiliza wananchi hao wakulima (wavamizi) na Wafugaji na kumaliza mgogoro huo Mkuu wa Mkoa Gaguti aliunda timu ya wataalam kupitia nyaraka mbalimbali kuhusu kijiji hicho na kuwasikiliza wananchi pande zote mbili ili kubaini ukweli na chanzo cha mgogoro ambapo timu hiyo ilifanya kazi yake na kuwasilisha majibu kwake.
Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kupitia taarifa ya timu aliyoiunda na kuwasili Kijijini Kahundwe na kusikiliza pande zote mbili za Wakulima (Wavamizi) na wafugaji aliwaeleza wananchi hao kuwa tayari Serikali ilishabaini ukweli wa ni nani mmiliki halali wa eneo hilo la Kijiji cha Kahundwe kati ya Wakulima na Wafugaji.
“Mwaka 1987 mamlaka za vijiji vinne zilikaa na kukubaliana kutenga eneo la kufugia mifugo yao na lilitengwa eneo la Kijiji Kahundwe kuwa eneo la wafugaji na kusajiliwa kisheria, lakini kuanzia mwaka 2008 hadi 2015 baadhi ya wananchi kutoka maeneno mengine walivamia eneo hilo na wavamizi sita walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kupatikana na hatia na kufungwa jera miezi sita kila mmoja.” Alieleze Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Mkuu wa Mkoa Gaguti aliendelea kuwaeleza wananchi kuwa tangu wakati huo kumekuwa na uvamizi wa wakulima kutoka nje ya Kijiji hicho na kuleta mgogogro mkubwa kati yao na wafugaji. Aidha, alisema kuwa Serikali tayari imebaini ukweli wa uhalali wa nani anatakiwa kuwa katika eneo hilo na itasimamia ukweli huo wa mwaka 1987 na kama kutakuwa kuna wananchi wanataka mabadiliko wafuate sheria kama wenzao walivyofanya katika kutenga eneo hilo kuwa la wafugaji.
“Hapa hakuna mgogoro wa ardhi bali ni uvunjifu wa sheria tu, nitahakikisha namaliza uvunjifu huu kuanzia sasa na sitaki kusikia jambo hili linaendelea. Lengo la kuja hapa ni kusimsmia msimamo wa Serikali kwa njia ya amani na utulivu. Natambua kuwa kuna wakazi au wafugaji 200 lakini 43 kati ya hao ni wavamizi si wenyeji nataka jambo hilo liishe mara moja.” Alitoa msimamo wa Serikali Mkuu wa Mkoa Gaguti.
MAAGIZO
Mkuu wa Mkoa Gaguti alimwagiza na kumpa wiki moja Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kuanzia tarehe 27/02/2019 kufanya uhakiki na utambuzi wa wafugaji wadogo ambao walisajiliwa katika Kijiji hicho cha Kahundwe na kuwaondoa wavamizi ambao ni wakulima na wafugaji wakubwa waliotoka maeneo mengine.
Pili Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka na timu yake wafanye uhakiki wa mifugo ili kubaini wafugaji ambao kwanza si raia wa Tanzania na pili kubaini wingi wa mifugo kusudi kama kuna wafugaji wakubwa wenye mifugo mingi waondolewe ili wafuate sheria za kuomba vitalu vya kufugia kama wafugaji wakubwa au wawekezaji katika vitalu.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kahundwe walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuwa mgogoro huo unachochewa na Diwani wa Kata ya Chanika kwasababu wakati wa Kampeini ya mwaka 2015 aliwahidi baadhi ya wananchi hao wavamizi kuwa akipata madaraka atahakikisha wanalichukua eneo la Kijiji cha Kahundwe kama eneo lao la kilimo.
Naye Bw. Bernard Sau Afisa Ardhi Wilaya ya Karagwe akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa kijiji cha Kahundwe kilisajiliwa mwaka 1987 kwa GN namba 620 kama Kijiji cha wafugaji na wakati huo ilikuwa Wilaya moja ya Karagwe kabla ya kutengwa Wilaya mbili za (Karagwe na Kyerwa) na baada ya kutenga Wilaya mbili kijiji cha Kaundwe kilibaki Wilaya ya Karagwe na kijiji hicho kina jumla ya Hekta 20,000 za kufugia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa