• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

RC Kagera Azindua Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru Na 57 ya Jamhuri Kwa Kuwaongoza Wananchi Kufanya Usafi na Kujitolea Kuchangia Damu

Imewekwa : December 4th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaongoza wananchi , Viongozi wa Taasisi mbalimbali  za Serikali na zisizo za Serikali na watumishi walio chini ya taasisi hizo kufanya usafi katika soko kuu la Bukoba  na kuchangia damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Mara baada ya kushiriki usafi ndani na nje ya Soko Kuu la Bukoba Mkuu wa Mkoa Gaguti aliongea na wananchi waliokusanyika kufanya usafi pamoja naye na kuwaeleza maudhui ya  maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaeleza kuwa mwaka huu 2019 maadhimisho hayo yanaadhimishwa Kanda ya Ziwa ambapo mikoa miatano inashiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali.

“Maadhimisho hayo yanaadhimishwa Kitaifa Mkoani Mwanza ambapo na mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita inashiriki  na mkoa wetu wa Kagera sisi tumezindua rasmi maadhimisho hayo  leo kwa  kushiriki pamoja na wananchi kufanya usafi wa soko letu  pia kujitolea damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa wahitaji ili kunusuru maisha yao.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti

Vilevile aliwaeleza wananchi hao kuwa wabunifu katika biashara zao ili kukuza uchumi na kipato chao lakini wakiwa wazalendo wa nchi yao, na aliwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa nchi yake na kutumia fursa ya uwepo wa nchi jirani za Rwanda, Burundi Uganda , Congo DRC na Sudani Kusini kufanya biashara na kuufanya mkoa wa Kagera kukua zaidi kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaeleza wananchi hao kuwa Mkoa wa Kagera unayo sababu kubwa ya  kusherehekea na kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri mkoa umenufaika kupitia katika Sekta ya mbalimbali akitaja chache alisema kuwa tayari Serikali ya Awamu ya Tano mkoani Kagera  imejenga Vituo 14 vya Afya kwa shilingi bilioni 5.9 Hospitali tatu za Wilaya kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5

Sekta ya Miundombinu Meli ya MV Victoria inakarabatiwa kwa gharama ya shilingi bilioni 22.8 na mwakani 2020 mwezi Machi inaanza safari zake tena katika Ziwa Victoria kutoka Mwanza kwenda  Bandari za Bukoba na Kemondo.  Katika Sekta ya Elimu tayari Serikali imetoa  jumla ya shilingi bilioni 3.4 Kukarabati shule kongwe za Kahororo, Bukoba, Kagemu na Rugambwa na ukarabati unaendelea.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaongoza wananchi na viongozi mbalimbali kuchangia  damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ambapo mpaka anaondoka katika eneo hilo tayari chupa 63 zenye ujazo wa nusu lita za damu zilikuwa zimekusanywa malengo yakiwa ni kukusanya chupa 400 kwa siku hiyo tu.

Kilele cha Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni tarehe 9 Desemba 2019 Mkoani Mwanza na Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni “Miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri: Uzalendo, Uwajibikajina Ubunifu ni Msingi wa Ujenzi wa Uchumi na Taifa letu.”

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa