- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea na kukagua shughuli za uvuvi katika soko la dagaa la kimataifa la Katembe-Magalini lililopo Kijiji Katembe, Kata ya Nyakabango, Wilaya ya Muleba.
Akizungumza na wavuvi na wananchi mara baada ya kukagua shughuli hizo, amewaeleza kuwa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali imeweka mpango wa kuwawezesha wavuvi kufanya shughuli zao kwa tija ili kunufaika na sekta hiyo. Na kubainisha jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha wavuvi hao kwa kutoa boti kwa vikundi vya wavuvi hao.
“Serikali yenu inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka utaratibu mzuri kupitia Wizara ya Mifugo na uvuvi ya kuwawezesha nyinyi kufanya shughuli za uvuvi hapa kwenye soko hili. Kuna maelekezo nimeyatoa kwa Halmashauri, kuna maelekezo nimeyatoa kwa mamlaka ya bandari yote haya ni kuwezeshe eneo hili kuwa la kimkakati,” ameeleza Mhe. Majaliwa
Aidha,ameitaka Mamlaka ya Bandari na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kukaa na kukubaliana kuwa na tozo inayofanana katika kuwatoza wavuvi na wafanyabiashara wa Mazao ya samaki wanaohifadhi bidhaa zao kwani Serikali ni moja
Pamoja na hayo amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kumuweka mtumishi wa aliyeajiriwa kukusanya mapato katika soko hilo ili iweze kumwajibisha pale atakapokiuka taratibu za kiutumishi achukuliwe hatua na si kumuweka kibarua akusanye mapato ya soko hilo linaloingizia Halmashauri fedha nyingi
Akijibu hoja za wananchi ameutaka uongozi wa Halmashauri kutenge fedha za kutengeneza barabara ya lami inayoelekea katika soko hilo, kununua taa kwa ajili ya usalama na kuboresha mazingira kwani mapato wanayokusanya yanaweza kuboresha mazingira ya soko hilo. Na kumtaka Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Bandari Tanzania aboreshe jengo la kupumzikia/kusubiria abiria na gati.
Sambamba na hayo amekemea juu ya uvuvi haramu na kuwataka wavuvi hao kufanya uvuvi wenye tija kwa maendeleo ya vizazi hadi vizazi
Akitoa maelezo mafupi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Dkt. Peter Nyanja ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/23 jumla ya tani milioni 26.96 za mazao ya dagaa zilikusanywa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa