- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa aanza rasmi ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Kagera akitarajia kutembele, kukagua, kuzindua au kuweka mawe ya msingi katika miradi kumi yenye thamani ya shilingi bilioni 927.3.
Mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera Septemba 18, 2021 Wilayani Biharamulo katika eneo la Nyakanazi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa mradi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo ynayosafirisha mizigo kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na Congo DR ambapo mradi huo ukikamilika utagharimu takribani shilingi bilioni 2.6
Akiwa katika mradi huo na kukagua hatua ya utekelezaji wa mradi iliyofikiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hakuridhishwa na kasi ya Mkandarasi katika ujenzi kwani mradi ulitakiwa kuwa umekamilika mwezi Machi 2021 lakini hadi sasa mradi bado upo asilimia 47 tu ambapo Waziri Mkuu alitoa alimwagiza Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge kusimamia kwa karibu mradi huo ukamilike ifikapo Novemba 23, 2021.
Aidha, akiongea na wananchi wa Nyakanazi Wilayani Biharamulo Waziri Mkuu Kassim majaliwa alisema kuwa Serikali inao mpango wa kulifanya eneo la Nyakanazi kuwa eneo la kimkakati kwa kuwa linapokea malori mengi ya mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi jirani na kutoka nchi hizo kwenda Bandari ya Dar es Salaam na kukifanya eneo hilo kuwa kituo kikubwa cha biashara.
Pia Waziri Mkuu aliuwagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kulipangilia vizuri eneo la Nyakanazi na kulipima kwa kuwa ni eneo linalokaliwa na watu wengi na wananchi wanatakiwa kujenga kwa utaratibu na kuruhusu miundombinu mingine kupangiliwa vizuri ili kupanya Nyakanazi kuwa kitovu cha baiashara.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahakikishia wananchi wa Nyakanazi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan itajenga upya barabara ya Rusahunga Nyakahura Rusumo kwani barabara hiyo imeisha muda wake, ikiwa ni pamoja na barabara ya Nyakanazi Kibondo kilometa hamsini kukamilishwa ili Nyakanazi ifikikie kwa urahisi.
Katika namna ya kipekee wananchi wa Nyakahura Mzani Wilayani Biharamulo wamehaidiwa kujengewa shule mpya baada ya kuwasilisha kilio chao kwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliposimama kuwasalimia katika eneo la Nyakahura mzani akielekea Wilayani Ngara ambapo shule iliyopo sasa imezidiwa uwezo na kupelekea watoto kusoma kwa shida. Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ataendelea na ziara yake Mkoani kagera Wilayani Ngara Septemba 19, 2021.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa