- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Vodafone Foundation wameanzisha mfumo maalumu wa M-MAMA unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Akizindua mfumo huo Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Toba Nguvila amesema kuwa viongozi wa mkoa wanatakiwa kuunga mkono mpango huo ili kuweza kuokoa maisha ya mama na mtoto.
"Hii ni huduma muhimu sana ya kuhakikisha akina mama anakuwa salama katika kipindi cha ujauzito na kuhakikisha anakuwa salama. Rais Samia amekuwa akituagiza tufanye jitihada kuhakikisha hakuna kifo kinatokea kwa mama wakati anajifungua na hakuna mtoto anayefariki kwa sababu zinazothibitika" ameeleza Ndg. Nguvila
Aidha amesema kuwa Mkoa wa Kagera pamoja na kamati zake kwa kushirkiana na wadau wa maendeleo umepiga hatua katika kupunguza vifo vya mama kutoka vifo 55 kwa mwaka 2020 hadi vifo 42 kwa mwaka 2022 na kwa mwezi Januari mpaka mwezi Machi mwaka huu vimetokea vifo 13.
Sambambana na hilo amesema viongozi wa Halmashauri wanatakiwa kutenga fedha la kutosha kuwasaidia akina mama wajawazito wanaopoitaji msaada wa kwenda kujifungua huku akisisitiza kuwa wataingia mikataba na watu binafsi wenye magari yatakayotumia kama magari ya kusafirishia wagonjwa ili kuwasaidia pale uhitaji unapokuwepo kwani mkoa huo una upungufu wa magari hayo.
Bi. Neema Kyamba Mratibu wa mama na mtoto mkoa wa Kagera alisema kuwa zimekuwepo sababu mbalimbali zinazopeleka vifo kwa mama na mtoto ikiwa pamoja na uwezo mdogo kwa watoa huduma za uzazi kwa mama na mtoto, uzembe pamoja na uchache wa watumishi katika vituo vya afya suala linalopelekea kuelemewa wateja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa