• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Ujio wa Madaktari Bingwa na Kliniki Tembezi Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Kuanzia Tarehe O5 Hadi 11 Novemba, 2018

Imewekwa : November 1st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti anapenda kuwataarifu Wananchi wa Mkoa wa Kagera na nje ya Mkoa kuwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wameandaa Kliniki tembezi ya Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Government) kuanzia tarehe 05 – 11 Novemba, 2018.

Ikiwa ni mara ya pili kutekeleza zoezi hilo la huduma za kibingwa katika Mkoa wa Kagera kutakuwa na Madaktari Bingwa kati ya 28 hadi 34 kutoka Hospitali za Kanda za Bugando, KCMC, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya,  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na baadhi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa. Madaktari hao Bingwa wanatarajia kutoa huduma katika magonjwa ya Uzazi na kizazi kwa wanawake, Magonjwa ya upasuaji kwa jumla, Magonjwa ya njia ya mikojo ikiwemo tezi Dume, Magonjwa ya pua, sikio na koromeo.

Magonjwa mengine yatakayoshughulikiwa na Madaktari Bingwa ni pamoja na Magonjwa ya mifupa, Magonjwa ya moyo, Magonjwa ya ndani ikiwemo sukari na figo, Magonjwa ya watoto, Magonjwa ya Afya ya kinywa na meno, Magonjwa ya macho, Magonjwa ya Ngozi, Magonjwa ya afya ya akili, na Saratani ya Mlango wa kizazi.

Mkuu wa Mkoa Gaguti anatoa rai kwa wananchi hasa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kuchangamkia fursa ya Madakitari Bingwa kwani gharama za kuwaona Madaktari hao zitakuwa nafuu sana ukilinganisha na gharama za kuwafuata Madaktari Bingwa Katika Vituo vyao vya kazi kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya Bugando au KCMC Moshi ikiwa ni pamoja na gharama za kusafiri na kuishi huko wakati ukisubiri kumuona Daktari Bingwa.

Mkuu wa Mkoa Gaguti anasisitiza kuwa (Mwananchi) mgonjwa kumuona Daktari Bingwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera itakuwa ni shilingi 10,000/= (Elfu kumi tu) kwa magonjwa yote isipokuwa magonjwa ya moyo itakuwa ni shilingi 15,000/= (Elfu kumi na tano tu). Gharama hizi ni nafuu sana ukilinganisha na gaharama ya shilingi 25,000/= hadi 40,000/= kumuona Daktari Bingwa akiwa katika kituo chake cha kazi kwa magonjwa yote na magonjwa ya moyo shilingi 40,000/= hadi shilingi 50,000/=.

Aidha, gharama za upasuaji nazo zitakuwa nafuu sana, upasuaji katika magonjwa yote gaharama yake itakuwa katai ya shilingi 60,000/= hadi 100,000/= tu ambapo itakuwa nafuu sana ukilinganisha na gharama za upasuaji Madaktari Bingwa wakiwa katika vituo vyao vya kazi ambapo huanzia shilingi 300,000/= hadi shilingi 1,500,000/=.

Pia Mhe Gaguti anawakumbusha wananchi kuwa zoezi la kuwaleta Madaktari Bingwa Mkoani Kagera kwa kiasi kikubwa litagharamiwa na Serikali ili kuhakikisha wananchi wake wanasogezewa huduma za matibau karibu.

“Katika zoezi tulilotekeleza Septemba 18 hadi 24, 2017 tuliweza kuwahudumia wananchi takribani 3,146 na mwaka huu 2018 tumelenga kuwahudumia wananchi 4,000 hadi 5,000 kwa kuwa tumeongeza wigo wa Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na tunatarajia wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo nao watapata  huduma za kibingwa.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Mwisho Mkuu wa Mkoa Gaguti anatoa Wito kwa wananchi ambao wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo, na Serikali ya Mkoa wa Kagera  imejipanga vizuri katika Dawa, vipimo, na katika utoaji wa huduma ili kuhakikisha Madaktari  Bingwa wanawahudumia wananchi kwa uhakika na kikamilifu zaidi.

Wananchi wenye matatizo ya kiafya wajitokeze kwa wingi ili kupata huduma za kibingwa lakini pia kwa kuwa muda utakuwa mfupi wa siku saba tu kuanzia tarehe 5 hadi 11, Novemba, 2018 wananchi mnakumbushwa kuwahi kuanzia tarehe 5 Novemba, 2018.


Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa