• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Taarifa Wwa Umma Kuhusu Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Kagera Tarehe 23 Aprili, 2019

Imewekwa : April 23rd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti anawajulisha wananchi wote wa Kagera kuwa Mkoa utapokea Mwenge wa Uhuru tarehe 24 Aprili, 2019 katika eneo la Murusagamba mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Kagera na baadae Mwenge wa Uhuru utaanza mbio zake katika mkoa wa Kagera katika Wilaya ya Ngara.

Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa Mkoani Kagera unatarajiwa kuzindua, kuweka Mawe ya Msingi, na Kukagua miradi ya maendeleo jumla 74 yenye thamani ya shilingi bilioni 18,894,323,585.90 Ambapo katika fedha hizo Serikali Kuu imechangia shilingi bilioni 10,262,407,160.86 sawa na asilimia 54.31%. Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba zimechangia shilingi milioni 282,853,162.91 sawa na asilimia 1.5%. Wahisani wamechangia shilingi bilioni 2,472,529,017.96 sawa na asilimia 13.09%. Pia wananchi wamechangia shilingi bilioni 5,876,534,244.17 sawa na asilimia 31.10%.

Miradi 74 ya Maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Kilimo, Barabara, Ujasiliamali kwa Watu wenye ulemavu Vijana na Wananwake, Viwanda, Mapambano dhidi ya Rushwa na Madawa ya Kulevya itatembelewa, kukaguliwa, kuzinduliwa na Kuwekewa Mawe ya Msingi na Mwenge wa Uhuru Mkoani Kagera. Aidha, Miradi 21 itazinduliwa, Miradi 12 itawekewa Mawe ya Msingi, na Miradi 38 itatembelewa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru pia miradi 3 ni ya shughuli nyinginezo.

Aidha, Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019 ni “Maji ni Haki ya Kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”. Kauli mbiu hii inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji na kutunza mazingira kama ilivyo haki ya kila mtu kupata maji na iwe haki ya kila mtu kutunza vyanzo vya maji ili kurahisisha upatikanaji wa maji.

Pia, Mkoa wa Kagera tayari umeanza na unaendelea kuwahamasisha wananchi pamoja na vijana ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 (umri wa kupiga kura) ili washiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2019. Mkoa wa Kagera unatarajia kuandikisha wananchi 1,277,776 watakaopiga kura katika vituo vipatavyo 3,798.

 

Pamoja na Kauli Mbiu tajwa hapo juu Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu zitaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, VVU/UKIMWI, Matumizi ya Dawa za Kulevya aidha, mapambano dhidi ya Malaria.

Mkuu wa Mkoa Gaguti anatoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Murusagamba Wilayani Ngara na maeneo yote ya mkoa Mwenge wa Uhuru utakapopita kutembelea, kukagua, kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi ili tuweze kupata ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2019 kuufurahia na kuushangilia Mwenge wa Uhuru kwa pamoja kama kiunganisho cha umoja wetu sisi Watanzania hasa Wanakagera ili tuendelee kuishi kwa amani, utulivu, upendo, umoja na mshikamano.

 

Mwenge wa Uhuru utapokelewa Murusagamba Wilayani Ngara tarehe 24 Aprili, 2019 na utakimbizwa katika Halmashauri za Wilaya zote za Mkoa wa Kagera ukianzia Ngara, Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Bukoba Manispaa, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Muleba na utahitimisha mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mei Mosi, 2019. Mimi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti nitaukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita tarehe 2 Mei, 2019.

Mwenge wa Uhuru karibu Mkoani Kagera ewe mwananchi shiriki katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, “Maji ni Haki ya Kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.


Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa