- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika siku yake ya kuzaliwa tarehe 29 Septemba, 2019 aliwaomba wananchi Mkoani Kagera kuendelea kumwombea afya njema Mhe. John Pombe Magufuli ili aendelee kuchapa kazi na kuufanya Mkoa wa Kagera uendelee kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai hiyo Septemba 29, 2019 katika viwanja vya Nyamkazi Manispaa ya Bukoba akiongea na wananchi wa eneo hilo ambao ni wavuvi wakiwakilisha wananchi wa mkoa wa Kagera ambapo alieleza namna Rais Magufuli alivyotekeleza miradi ya maendeleo katika mkoa huo na kustahili pongezi ikiwa ni pamoja nakuendelea kumwombea sala ili aendelee kutekeleza maendeleo kwa wnanchi wa Kagera
“Sisi Wanakagera tunayo sababu ya kumpongeza Rais Magufuli katika siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 29/10/2019 kwani Serikali yake ya Awamu ya Tano imetekeleza miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Kagera yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 151 tangu aingie madarakani mwaka 2015.” Alieleza Mkuu wa Mkoa Gaguti
Mhe. Gaguti alifafanua kuwa miradi iliyopokea fedha na kutekelezwa ni pamoja na shilingi bilioni 4.5 ujenzi wa Hospitali za Wilaya tatu, bilioni 5.9 ujenzi wa vituo vipya 14 vya afya, bilioni 22 ujenzi wa chuo cha Ufundi stadi VETA Kagera, bilioni 3.2 ukarabati wa shule kongwe, bilioni 92.6 ujenzi wa meli mpya, bilioni 22.8 ukarabati wa meli ya MV Victoria uliofikia asilimia 53. Aidha, huduma ya upatikanaji wa dawa muhimu umeimarika nchini hadi asilimia 97% kutoka shilingi milioni 800 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi bilioni 5.4 mwaka huu 2019.
Pia Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwahimiza wananchi wa Nyamkazi ambao shughuli zao ni uvuvi kujitafakari wao weyewe katika kazi zao na kuona namna bora ya kujiunga katika vikundi na kuanza kutafuta masoko ya mazao ya samaki katika nchi jirani na mkoa wa Kagera na kuacha ndoto za kuwasubiri wawekezaji kutoka nje ya mkoa wakati wao wapo na shughuli zao ndizo hizo za kila siku.
“Nataka kuona viwanda vya samaki hapa Kagera kwani fursa ya kupata mazo ya samaki tunayo lakini pia nataka niione Kagera ikishindana na nchi ya Rwanda kwani ukiangalia ukubwa wa nchi ya Rwanda ni kilometa za mraba 26000 wakati Mkoa wa Kagera unazo kilometa za mraba 25000 pia mkoa wetu unazo fursa nyingi za kutosha kushindana na nchi ya Rwanda, wavuvi tutoke tukatafute masoko tuache kujifungia ndani wenyewe mwisho wa siku tukakuze mitaji yetu.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti
Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa wazalendo kwa kuzilinda raslimali za nchi kwa kutoshiriki uvuvi haramu pia kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wananchi hao wanapoona au kupata taarifa za mtu yeyyote anayeshiriki kwenye vitendo viovu vya uvuvi haramu hasa katika Ziwa Victoria.
Mwisho Mhe. Gaguti aliupongeza uongozi wa Kituo cha Ulinzi na Usimamizi wa Raslimali za Uvuvi Mkoa wa Kagera kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuhakikisha uvuvi haramu haufanyiki katika Ziwa Victoria aidha, kufanikiwa kunasa zana haramu ambazo ni nyavu za kuvulia samaki zisizoruhusiwa au kukidhi viwango zenye thamani ya shilingi 1,821,200,000 ambapo aliongoza zoezi la kuzichoma moto zana hizo haramu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa