- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Benki ya NMB Yazindua Tawi Jipya Kaitaba Manispaa ya Bukoba
Benki ya NMB yazindua tawi jipya katika Manispaa ya Bukoba ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma zake kwa wateja wa benk hiyo. Tawi jipya la Benki ya NMB lijuliknalo kwa jina la KAITABA lilizinduliwa Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Oktoba 4, 2017.
Katika uzinduzi huo wa tawi jipya la Kaitaba pia Mkurugenzi wa NMB Tanzania Bi Ineke Bussemaker alihudhuria ambapo alisema kuwa tangu kubinafsishwa kwa Benki ya NMB miaka 12 iliyopita tawi la Kaitaba ni tawi la 211 kutoka matawi 100 yaliyokuwepo awali nchi nzima.
Bi Ineke alisema Benki hiyo imepiga hatua kubwa za kimaendeleo tangu kubinafsishwa miaka 12 iliyopita kwani hadi sasa Benki hiyo ina Mawakala zaidi ya 3800 nchi nzima. Aidha alisema kuwa tayari Benki hiyo inatoa huduma za internet kuwa wateja wao ambapo wanaweza kutoa fedha popote walipo bila kufika katika Benki.
Pia Bi Ineke Alisema kuwa Benki ya NMB tayari ipo kwenye soko la hisa na hisa zake zinapanda kila siku pia tayari hisa hizo zina wateja zaidi ya milioni 2. “Benki ya NMB kwasasa ni benki bora afrika na tumepata cheti cha ubora .” Alisistiza Bi Ineke.
Aidha, Bi Ineke alitoa ufafanuzi wa kwanini limeongezwa tawi jipya katika Manispaa ya Bukoba kuwa ni kutokana na maombi ya wateja wao kuwa hapo awali huduma zilikuwa haziendi kama matarajio ya wateja wao na wao kama benki wakaamua kutekeleza maombi ya wateja kwa kuongeza tawi la Kaitaba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akizindua tawi la Kaitaba aliwashukuru Uongozi wa Benki ya NMB kuongeza tawi jipya mjini Bukoba na aliwaasa wajasiliamali kutumia fursa hiyo kuongeza mitaji yao kupitia Benki ya NMB tawi la Kaitaba.
Aidha, Mhe Kijuu alitoa wito pia kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera hasa Manispaa ya Bukoba kuchangamkia huduma ya chap chap iliyoanzishwa na Benki ya NMB ili kupata huduma za kifedha kwa wakati na kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa