- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha kampeni ya TUWAJIBIKE yenye lengo la kuwahimiza wafanyabiashara kutumia mashine za risiti za kieletroniki ili kukuza maendeleo kupitia kodi
Akizundua kampeni hiyo, katika viwanja vya soko kuu la Manispaa ya Bukoba, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa ameeleza juu ya umuhimu wa ulipaji kodi kwa maendeleo ya Taifa letu na kuwataka wafanyabiashara kutumia mashine za kieletroniki ili Serikali iweze kupata kodi inayowezesha kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, barabara, umeme na nyinginezo
“Leo nimezindua kampeni ya TUWAJIBIKE katika Mkoa wa Kagera, lengo ni kuhimizana kulipa kodi. Kwenye hili sitakuwa na huruma, kwenye kodi lazima tulipe kodi kwani hata Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameagiza tusimamie na kuhakikisha wafanyabiashara tunalipa kodi, niwaombe sana tulipe kodi,” ameeleza Mhe. Mwassa
Ameendelea kueleza kuwa mfanyabiashara anatakiwa kulipa kodi na mfanyakazi analipa kodi kupitia mshahara wake. Mkoa wa Kagera unapoteza mapato mengi kwani biashara nyingi hazijarasimishwa. Wafanyabiashara walio wengi wanapanga bidhaa kandokando mwa barabara hivyo kuipa ugumu mamlaka ya mapato kukusanya kodi kwa wafanyabiashara hao
Katika mkutano huo ameeleza juu ya fursa iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya mifugo, Mpango wa kopa ng’ombe lipa maziwa, wataletwa ng’ombe wengi ambapo kwa Mkoa wa Kagera imetengwa dola milioni 30 sawa na Tsh. bilioni 70 kwa ajili ya Mpango huo. Na Taasisi ya Bill and Melinda Gates (BMGF) wakaongeza dola millioni 7 hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kila familia kuwa na mradi wa ufugaji ng’ombe wa maziwa
Akitoa maelezo juu ya kampeni hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Kagera Ndg. Ayub Mwita ameeleza kuwa uzinduzi wa kampeni ya TUWAJIBIKE yenye kauli mbiu “Kodi Yetu Maendeleo Yetu” maana yake ni ukuaji wa haraka wa maendeleo ya Nchi yetu yanatokana na kodi zetu zinazolipwa. Hivyo Watanzania bila kulipa kodi Nchi haiwezi kujitegemea na kujiletea maendeleo ya haraka.
Kulipa kodi kunaiwezesha Serikali kujenga miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, kujenga hospital na vituo vya afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa