- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akitembelea Chama Kikuu cha Ushirika cha Karagwe Development Co operative Union Limited (KDCU LTD) akikagua na kujionea maandalizi ya ukusanyaji na ununuzi wa Kahawa kwa msimu mpya wa mwaka 2019/20 ili kutatua kero zilizojitokeza katika msimu uliopita wa 2018/19 zisijitokeze msimu huu.
Akiwa Wilayani Karagwe Mei 23, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti alikutana na Bodi na uongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika KDCU LTD na kufanya nao mazungumzo pia kupata taarifa ni jinsi gani chama hicho kimejiandaa kukuksanya na kununua kahawa kutoka kwa wakulima katika wilaya za Karagwe na Kyerwa.
Mara baada ya kufanaya mazungumzo na Uongozi na Bodi ya KDCU LTD Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaagiza wajumbe wa bodi kuhakikisha wanaondoa kero zilizojitokeza msimu uliopita 2018/19 ikiwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa fedha kuwafikia wakulima katika Vyama vya Msingi au fedha hizo kutumika kabla ya wakati akimaanisha fedha za wakulima kuingizwa katika matumizi ya Chama Kikuu cha Ushirika kabla mkulima hajalipwa.
Pili, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaagiza KDCU LTD kuhakikisha wanakuwa na mpango mkakati ulio thabiti wa kupata fedha mapema kabla ya kukusanya kahawa ya waulima katika vyma vya msingi ili kuondoa kero za ucheleweshaji wa fedha na kupelekea wakulima kuuza kahawa yao kwa njia ya magendo ili kupata fedha ya kujikimu.
Tatu, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwataka KDCU LTD kuhakikisha wanatoa ushirikiano thabiti kwa Serikali ili kudhibiti magendo ya kahawa kwa kuondoa kero zote za mwaka jana zilizopelekea wakulima baadhi yao kuuza kahawa kimagendo kwa kuweka mfumo thabiti wa kupata fedha na fedha hizo kumfikia mkulima kwa wakati mara baada ya kukusanya kahawa yake katika chama cha msingi.
Katika hatua nyingne Mkuu wa Mkoa Gaguti alitembelea shamba bora la mkulima wa Kahawa Katika Kijiji cha Katembe Kitongoji Kibugu Kata Kituntu ambapo aliwataka wakulima wa Kahawa kuhakikisha wanazalisha kahawa bora kwa kuvuna kahawa iliyokomaa na kuanika kwa kuzingatia ubora ili kahawa hizo zipate bei nzuri kwenye soko la dunia
Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaagiza viongozi wa Vyama vya Msingi kuacha tabia ya kutumia fedha za wakulima katika matumizi ya vyama vyao kabla ya fedha hizo kumfikia mkulima. Pia aliwataka wakulima kufungau akaunti katika taasisi za kifedha kama benki ili malipo ya fedha zao yafanyike moja kwa moja katika akaunti zao na kuondoa migogoro ya fedha kupita katika mikono mingi kabla ya kuwafikia.
Mwisho Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwa wananchi ambao ni wakulima wa kahawa kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kupambana na biashara ya magendo ya kahawa kwa kutoa taarifa katika Serikali. Pili aliwataka Makarani katika vyama vya msingi kuhakikiaha wanapima kahawa ya wakulima kwa usahihi ikiwa ni pamoja na pointi kuziandika katika kilo za mkulima ili kuondoa malalamiko ya wakulima kuibiwa kahawa yao katika mizani.
“Sisi tayari tumejipanga vyema Serikalini kudhibiti magendo ya kahawa na tuhakikisha kila kahawa itakayokamatwa inataifishwa na fedha itakayokuwa inapatikana asilimia 30% tutaitoa kama zawadi ya mtoa taarifa, pili asilimia 50% tutaitoa kwa vijana watakokuwa wanashiriki katika ukamataji wa kahawa ya magendo.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Naye Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Kagera Bw. Robert Kitambo alisema kuwa katika msimu huu wa mwaka 2019/20 vyama vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vinatarajia kukusanya kahawa kilo milioni 50 hadi 52 ikiwa KDCU LTD watakusanya kilo milioni 35 na KCU 1990 LTD watakusanya kilo milioni 12.6 na vyama vingine kukusanya kilo milioni 4.4 ambapo katika msimu uliopita wa mwaka 2018/19 zilikusanywa kilo milioni 58.9 za kahawa kwa mkoa mzima wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa