- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera waendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha mipaka yake na nchi jirani hasa kulinda ili kukuza uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla lakini pia kuhakikisha wahamiaji haramu hawaingii wala kuingiza mifugo yao nchini bila kufuata taratibu kanuni na sheria za nchi.
Ni baada ya Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera kutembelea na kukagua mipaka ya Tanzania na Uganda kuanzia Kakunyu hadi Mtukula Wilayani Missenyi ili kujionea changamoto mbalimbali katika mpaka huo ili hatua ziendelee kuchukuliwa kuimarisha mpaka huo.
Akitembele na kukagua mpaka huo Februari 27, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti na msafara wake walilazimika kuingia nchini Uganda na kurudi chini katika baadhi ya maeneo ili kuyafikia mawe ya mpaka yanayotenganisha nchi mbili za Tanzania na Uganda kutokana na upande wa Tanzania kutokuwa na barabara ya usalama ya mpaka ambayo inatakiwa kutoka Mtukula Wilayani Missenyi hadi Murongo Wilayani Kyerwa.
Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kutembelea na kukagua mawe ya mpaka namba 27 (Kakunyu), 28 (Kalola) na jiwe namba 29 Bugango alisema kuwa pamoja na kuwa Serikali ina mpango wa kutenga fedha za kujenga barabara ya usalama kwa upande wa Tanzania kutoka Mtukula hadi Kakunyu lakini mkoa kwa kuona changamoto ya mpaka huo utaanza kuchonga barabara kidogokidogo ili kupunguza kero ya kuingia nchi jirani wakati doria na ukaguzi wa mpaka ukiendelea.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alifanya mikutano ya hadahara na wananchi katika Vijiji vya Bugango, na Rwengiri Kata Kakunyu na kuwaeleza umuhimu wa kuwa wazalendo kulinda mipaka ya nchi yao na kutoa taarifa pale wanapogundua kuwa kuna wahamiaji haramu au watu kutoka nje ya nchi wameingia bila kufuata utaratibu na sheria za nchi.
Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza wananchi kuhakikisha wanautumia vizuri mfumo wa nyumba kumi za kiusalama kuhakikisha wanawabaini wahamiaji haramu na kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika pia kutowaficha wahamiaji haramu katika nyumba zao jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
“Nyinyi wananchi nawombezi sana kuwa wazalendo wa kwanza kwa kulinda mipaka ya nchi yenu, ulinzi wa mipaka ya nchi hautegemei Vyombo vya Ulinzi na Usalama peke yake bali na wananchi tunatakiwa kuwa wazalendo wa hali ya juu kwa kutoisaliti nchi yetu. Pia kama hatutotoa taarifa ya wahamiaji haramu ni kosa la jinai kufanya hivyo.” Aliwasisitiza wananchi Mkuu wa Mkoa Gaguti
Mwisho alivipongeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wilayani Missenyi kwa kuendelea kuilinda mipaka ya nchi vizuri na kuendelea kuondoa wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kufuata sheria za nchi lakini pia na kuondoa mifungo inayoingizwa wilayani humo kinyemera ili kupatiwa marisho kutoka nchi jirani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa