- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kwenda kwenye maeneo ya wananchi kwa ajili ya kutoa huduma,kusikiliza kero zao na kuzitatua
Amesema hayo katika Kijiji cha Nyakanazi Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akiwa njiani kuelekea wilayani Ngara kuwasha umeme vijijini na kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Nishati kutoka nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda wanaohusika na Mradi wa umeme wa Rusumo utakaozalisha megawati 80
“Viongozi wenzangu tutoke maofisini na tuwafuate wananchi walipo,haina maana yoyote kama kuna kiongozi hapa na kuna shida ipo na haijawahi kutatuliwa, Mhe Rais anachotaka ni wananchi hawa kusikilizwa na kama kuna kero sisi tuzimalize kabla yeye hajaja,wananchi wakisema kuna shida sisi tuzimalize,yeye kazi yake kubwa ni kutafuta fedha kwa ajili ya maendeleo.” amesema Dkt.Biteko
Amesisitiza kuhusu matumizi sahihi ya fedha za Serikali ili wananchi wapate huduma stahiki na hivyo kuwapunguzia kero wanazopata wakati wakijiletea maendeleo
Ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupeleka umeme kwenye eneo la Kabulaishoke katika kijiji cha Nyakanazi baada ya viongozi wa eneo hilo kumweleza kuwa bado hakuna umeme; ambapo Mkurugenzi Mkuu wa REA,Mhandisi Hassan Saidy amemuahidi Naibu Waziri Mkuu kuwa, mkandarasi, kampuni ya Nakuroi ataanza kazi katika eneo hilo ndani ya mwezi mmoja
Ameagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa na mpango maalum wa kusambaza umeme kwenye eneo hilo la Nyakanazi kutokana na kupitiwa na miundombinu ya umeme kutoka kituo kikubwa cha umeme cha Nyakanazi ambacho kinasambaza kwenye maeneo mengine ya nchi
Katika hatua nyingine,Naibu Waziri Mkuu, amekagua kituo cha umeme cha Nyakanazi ambacho kitapokea umeme kutoka mradi wa wa umeme wa Rusumo kupitia njia ya msongo wa kV 220 na kusambaza kwenye maeneo mbalimbali ya nchi
Akiwa kituoni hapo, Dkt. Doto Biteko amezungumza na vijana wa kitanzania wanaoendelea na ujenzi wa eneo kutakapowekwa mtambo wa kupoza umeme kabla ya kuwasambazia wananchi ambapo amewaeleza vijana hao kuwa kazi wanayofanya ni kwa heshima ya Nchi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa