- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa awakumbusha viongozi wa dini ya Kiislam Manispaa ya Bukoba kuendelea kudumisha amani mshikamano na kuwahimiza wananchi kuendelea na ushirikiano, upendo na amani hususani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili mkoa uendelee kupaa kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa aliyasema hayo katika semina fupi ya viongozi wa dini ya Kiislam iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera Machi12, 2025 akiwakutanisha Maimamu wa Misikiti yote ya Manispaa ya Bukoba. wakiongozw na Sheikh Haruna kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera.
"Katika mkoa kukiwa na magomvi, kelele na kutoelewana baina ya viongozi kwa viongozi au viongozi na waumini mkoa hauwezi kutulia na maendeleo yatasuasua, lakini nawashukuru viongozi wa madhehebu ya dini zote mkoani kagera kwa mshikamano na umoja jambo ambalo limepelekea kuleta maendelo chanya kwa wananchi wa Kagera" Alisistiza Mkuu wa Mkoa Mwassa.
Akitaja mafanikio yaliyofikiwa kutokana na utulivu wa mkoa na maombezi ya viongozi wa dini Mkuu wa Mkoa Mwassa alisema Mkoa umefanikiwa kupata fedha za kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo itakayochachua uchumi wa mkoa na wananchi kwa ujumla. Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa soko Kuu la Bukoba na Stendi kuu ya Bukoba,Ujenzi wa kingo za Mto Kanoni, Upanuzi wa barabara ya njia nne na ujenzi wa Stendindi ya mjini kati.
Miradi mingine ni pamija na ujenzi wa Ofisi mpya ya mkuu wa mkoa, Ujenzi wa Uwanja mpya wa ndege, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Bukoba, Upanuzi wa Bandari za Bukoba na Kemondo na ujenzi wa Kitega uchumi cha Machinga Manispaa ya Bukoba.
Naye Sheikh Haruna Kichwabuta, Sheikh wa mkoa wa Kagera katika semina hiyo aliwataka viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa kwa waamini wao ikiwa ni katika utoaji wa sadaka na zaka hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha, viongozi hao wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za maendeleo katika mkoa wa Kagera na sasa miradi mikubwa inatekelezwa ambayo ilikuwa imekwama kwa kipindi kirefu pia walimshukuru Mkuu wa Mkoa Hajjat Fatma Mwassa kwa uongozi madhubuti na usimamizi wa miradi ya maendeleo katika mkoa wa Kagera.
Katika semina hiyo Mkuu wa Mkoa Kagera Hajjati Fatma Mwassa alitoa sukari, mafuta ya kupikia, mchele, ngano na tende kwa Maimamu wa Misikiti yote ya Manispaa ya Bukoba ikiwa ni moja ya sadaka yake katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa viongozi hao wa dini ya kiislamu ili waendelee kutekeleza majukumu yao vyema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa