• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Wahifadhi wa Msitu wa Biharamulo Wakitoa Maelezo Kwa MKuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu waPili Kutoka Kulia

Imewekwa : August 22nd, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Atoa Maagizo Makali Kwa Wananchi na Watendaji wa Serikali Wanaoendelea Kukaidi Maagizo ya Rais Magufuli 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu afanya ziara katika Misitu ya Hifadhi ya Biharamulo na Nyantakala Wilayani Biharamulo kuona kama agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wavamizi wa misitu hiyo kuondoka mara moja alilolitoa tarehe 19 Julai, 2017 alipofanya ziara yake Mkoani Kagera.

Rais Magufuli akiwa Wilayani Biharamulo Julai 19, 2017 aliagiza wavamizi wote wa Misitu ya Asili na Wafugaji waliovamia Mapori ya Akiba kuhakikisha wanaondoka mara moja katika hifadhi na watakaokaidi  wachukuliwe hatua za kisheria.

Hatua hiyo ilitokana na operesheni ondoa mifugo iliyofanyika Mkoani kagera kunusuru Misitu ya asili, mapori ya akiba na vyanzo vya maji ambavyo vilikuwa vimevamiwa na kuharibiwa kwa kiwango kikubwa kwa kukata mkaa, kuendesha kilimo na kuingiza mifugo katika Misitu na Mapori ya Akiba.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu akitembelea Misitu ya Biharamulo na Nyantakala Wilaya Biharamulo Agosti 22, 2017 bado alikuta shughuli za uharibifu wa uchomaji wa mkaa katika misitu hiyo ukiwa unaendelea kwa baadhi ya wananchi wachache, pia waliokaidi kuondoka katika makazi waliyoyaanzisha katika Misitu hiyo jambo ambalo lilipelekea atoe maagizo makali kama ifuatavyo;

Mkuu wa Mkoa Kijuu alimwagiza Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kufikia tarehe 26 Agosti, 2017 awe amesitisha mara moja vibali vyote vya  umiliki na uvunaji wa miti kwenye mashamba ambayo yanamilikiwa na wananchi yaliyopo  jirani na Hifadhi za Misitu ya Biharamulo na Nyantakala kwa kuwa wamiliki hao wanayatumia mashamba hayo ya miti kama ngao huku wakifanya uhribifu wa uchomaji mkaa katika misitu hifadhi.

Agizo la pili, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpago Bw. Yasin Mahanga asimamie uvunjwaji wa matuta yanayozuia maji kupita katika mkondo wake kwenye bonde la msitu Nyantakala pia kuwaondoa wananchi wote wanaoendesha kilimo katika bonde hilo mara moja na kumzuia mwananchi anayewatoza fedha wafugaji kunywesha maji  mifugo yao katika lambo lililopo katika bonde hilo kuacha  tabia hiyo mara moja vinginevyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Agizo la tatu la Mkuu wa Mkoa Kijuu ni kwa wananchi waliovamia na kuanzisha makazi katika Msitu wa Nyantakala na kuyabatiza makazi hayo jina la MOMBASA RAHA kuondoka mara moja ifikapo tarehe 9 Septemba, 2017. Wasipoondoka wenyewe  hadi tarehe 10 Septemba, 2017 Mhe. Kijuu ameagiza Jeshi la Polisi kuvunja makazi hayo na kuwalazimisha wananchi wavamizi kuondoka kwa lazima.

Mhe. Kijuu anaendelea na ziara ya katika Mapori ya Akiba ya Burigi na Kasindaga kujionea mwenyewe kama agizo la Rais John Pombe Magufuli limezingatiwa na kutekelezwa kikamilifu.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa