• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Wakinamama Wajawazito Waonywa Kutochanganya Dawa za Kienyeji na Huduma za Kitaalam Wakati Wakisubiri Kujifungua Mkoani Kagera

Imewekwa : October 30th, 2018

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera unatoa rai na angalizo kwa Wakinamama Wajawazito Mkoani humo kuzingatia kanuni na ushauri wa kitaalam wanaopewa na wataalam wa masuala afya katika Hospitali hiyo na kuacha kuchanganya huduma za kitaalam na dawa za kienyeji kwa kunywa dawa hizo na kuchanganya dawa zilizoidhinishwa kisheria ili kujifungua salama na kwa haraka.  

Rai hiyo ilitolewa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera mara baada ya kupata kesi za mara kwa mara kwa Wakinamama Wajawazito kupasuka vizazi wakati wa kujifungua au watoto kuzaliwa wakiwa wamechoka sana jambo ambalo linasababisha watoto kuwa hatarini kupoteza maisha lakini pia hata mama mwenyewe anakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha yake.

Sababu kubwa inayosababisha Wakinamama hao Wajawazito kupasuka vizazi au watoto kuzaliwa wamechoka ni baadhi yao wanapopewa rufaa kutoka katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma kuja Hospitali ya Rufaa kujifungua wanakuja na dawa za kienyeji ambazo wanazipata mitaani kwa imani kuwa kuwa wakizitumia zitawasaidia kuongeza uchungu na kujifungua haraka na dawa hizo wanazitumia kwa uficho wakiwa Hospitali jambo ambalo ni hatari sana kwao wenyewe na mtoto tumboni.

 “Tumegundua tatizo hili mara baada ya kuona sisi watoa huduma tunatimiza wajibu wetu kwa kutoa huduma stahiki na sahihi kwa muda muafaka kwa Wakinamama Wajawazito na wakati mwingine Mama Mjamzito anakuwa anaendelea vizuri chini ya uangalizi wa watoa huduma wetu lakini ghafla hali inabadilika mama anapasuka kizazi au mtoto anazaliwa akiwa amechoka sana au wakati mwingine kusababisha kifo ndipo tuliamua kuanza kufanya utafiti sisi wenyewe ndani ya Hospitali.” Alifafanua Bw. Kiiza Kilwanila  Katibu wa Hospitali.

Bw. Kiiza alisema kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina waligundua kuwa Wakinamama Wajawazito wanakuja na dawa hizo za kienyeji zikiwa za kunywa, kutafuna au kupaka ili mama ajisikie uchungu haraka na ajifungue kwa muda mfupi na wamekuwa wakizificha jikoni wenyewe wanaita “Kijanjabi” na wanakuwa wanazitumia kwa kificho jambo ambalo linasababisha matatizo makubwa hadi kupelekea vifo vya mama mwenyewe, mtoto au wate mama na mtoto.

Bw. Kiiza alisema kuwa tarehe 29 Oktoba, 2018 Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera uliamua kuendesha msako ndani ya Hospitali ambapo walibainika Wakinamama Wajawazito sita wakiwa na dawa za kienyeji (Mushana, Kalandarugo) na nyinginezo wakitumia kwa uficho pamoja na huduma na wanazopewa na Wataalam wa Afya walioidhinishwa kisheria kutoa huduma za kitabibu katika Hospitali hiyo.

Imani hizo au matumizi ya dawa hizo za kienyeji ambazo hazikuidhinishwa kitaalamu yanarudisha nyuma juhudi za Serikali za kupunguza vifo vya Wakinamama Wajawazito na watoto na kusababisha vifo jambo ambalo linaweza kusababisha Mkoa wa Kagera kuonekana kuwa vifo vya Wakinamama Wajawazito na watoto vipo juu kumbe tatizo linasababishwa na akina mama wenyewe ambapo lawama zinaelekezwa  kwa Serikali na Watoa huduma hasa waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inasisitiza kupunguza vifo vya Wakinamama Wajawazito na Watoto lazima juhudi hizi za Serikali ziungwe mkono hasa Wakinamama Wajawazito kwa kuhakikisha Wataalam wa Afya wanatekeleza majukumu na wajibu wao wa kiweledi katika kutoa huduma na ushauri kwa wananchi.

Wito wa Uongozi wa Mkoa wa Kagera pamoja na Hospitali ya Rufaa ni wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupunguza vifo vya Wakinamama Wajawazito na Watoto kwa kutoa elimu ya kutosha kuwa mama anapofikishwa Hospitali mapema anakuwa katika mikono salaama  ya Wataalam wa Afya. Aaidha, wananchi waache imani potofu kuwa dawa za kienyeji zinasaidia katika kurahisisha mama mjamzito kujifungua, imani hizo zipuuzwe kwani zinasababisha madhara makubwa hadi kupelekea vifo vya mama na watoto.

Kama Wakinamama Wajawazito hawataacha tabia hiyo ya kuchanganya dawa za kienyeji na huduma za kitaalam uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera utachukua hatua kali kwa mama yeyote atakayebainika au kukamatwa ikiwa ni kutozwa faini au pia kuchukuliwa hatua za kisheria. Wito ni kuacha tabia hizi zisizo za busara, akina baba ni jukumu lenu pia kuwaelimisha wake zenu kuzingatia ushauri bora wa kitaalam ili kuachana na imani potofu ili mama na mtoto watoke salama katika chumba cha kujifungulia na kuendelea kujenga familia bora.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa