- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge awataka wananchi mkoani Kagera kuendelea kushikamana na kuilinda amani ya Tanzania kama ilivyokuwa tangu Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 hadi sasa mwaka 2021 Tanzania inapoadhimisha miaka 60 ya uhuru bila kuwa na mvurugano wala uvunjifu wa amani wa kuligawa taiafa la Tanzania.
Hayo yalisemwa na Profesa Faustin Kamzora ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania wakati akiwahutubia wananchi mkoani kagera yaliyoadhimishwa Kimkoa katika Uwanja wa Uhuru Manispaa ya Bukoba Desemba 8, 2021.
“Katika mambo yoote ambayo tunaweza kujivunia katika mkoa wetu wa Kagera na taifa kwa ujumla ni kuendelea kuishi katika hali ya amani na utulivu bila kupigana au kuwa na vitendo hatarishi vya kuvunja amani na mshikamano wetu kama watanzania, naomba wote tujipongeze na tuendelee kuitunza amani kama tulivyoanza wakati wa kupata uhuru mwaka 1961 alisema Profesa Kamzora kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera”.
Aidha, katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Charles Mbuge alisema kuwa pamoja na mkoa wa Kagera kupitia changamoto nyingi tangu uhuru mwaka 1961 za majanga ya magonjwa, Tetemeko, Ajali ya Meli na Ukame lakini Mkoa umepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbalimbali za maendeleo kama barabara, usafiri wa angina majini,Sekta za kilimo, Elimu, Uchumi na bado kagera inazidi kusonga mbele.
Wito wa Mkuu wa Mkoa Charles Mbuge ni kuona wanakagera wanaendelea kuchapa kazi na kukuza uchumi zaidi na kuzilinda afya zao ilikuweza kufika miaka 100 ya uhuru wa Tanzania. Kilele cha Maadhimisho ya uhuru nchini huadhimishwa kila mwaka Desemba 9, na Mwaka huu 2021 mikoa imeadhimisha kilele cha maadhimisho ya Uhuru Desesmba 8, ili kutoa mwanya wa Sherehe za Kitaifa zitakazoadhimishwa kitaifa Desemba 8, 2021
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa