• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Wananchi wa Mkoa Wa Kagera Mnasubiri Nini Kuchangamkia Fursa ya Hifadhi Tano Tarajiwa za Taifa

Imewekwa : September 11th, 2018

Wawekezaji wazawa Mkoani Kagera wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika Mapori ya akiba Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika yaliyotangazwa hivi Karibuni kuwa hifadhi za Taifa ambapo mapori hayo yalikuwa chini ya Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na sasa tayari  Mapori hayo yanasimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akiwa katika Pori la Burigi eneo la Nkonje mara baada ya kupita katika pori hilo na kujionea wingi wa wanyama pori mbalimbali ambao wameongezeka kwa kasi na uoto wa asili kurejea katika hali yake baada ya kuondolewa wavamizi na mifugo katika Mapori hayo.

Katika hatua za awali Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeanza mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa Mapori hayo ili kuyapandisha hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa Tanzania. Kwanza TANAPA imewaleta watumishi 16 Mkoani Kagera ili kurahisisha mchakato wa upandishwaji hadhi wa Mapori hayo na kuongeza doria kwa kishirikiana na watumishi waliokuwepo wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania TAWA.

Watumishi hao 16 wa TANAPA wanaongozwa na Bw. Damian Salu ambaye ni Mkuu wa Hifadhi na Mratibu wa mchakato wa upandishwaji hadhi wa Mapori ya Akiba matano Mkoani Kagera ambapo akiongea na Mkuu wa Mkoa Gaguti katika Pori la Burigi alisema kuwa pamoja na TANAPA kuwa na watumishi hao 16 lakini imeanza kuchukua mbalimbali hatua za kuboresha mapori hayo.

Bw. Salu alisema kuwa tayari TANAPA imeanza kutengeneza miundombinu ya barabara na  tayari Kilometa 35 za barabara zimerekebishwa ili kuweka urahisi wa Watalii wa nje na ndani kupita katika Hifadhi hizo kwa urahisi wakati wa kutalii. Pili ni kuongeza doria katika mapori hayo ili kukomesha ujangiri katika Hifadhi za Taifa tarajiwa.

Mikakati mingine ni kuelimisha wananchi wanaozunguka Hifadhi tarajiwa juu ya umuhimu wa kutunza Hifadhi na jinsi ya wao watakavyonufaika na Hifadhi hizo katika masuala ya maendeleo ya jamii pamoja na ulinzi shirikishi kati yao na Shirika la Hidhi za Taifa Tanzania. Aidha, TANAPA wanaendelea na mikakati ya kuzitangaza Hifadhi mpya zilizoko Mkoani Kagera ili wawekezaji wa ndani nje kuja kuwekeza Kagera.

Bw. Salu pia alisema kuwa TANAPA wanao mpango wa kupandikiza aina mbalimbali nyingine za wanyama katika Hifadhi tarajiwa ili kuongeza vivutio ambavyo ni muhimu kwa Watalii wa ndani na nje kuja katika Hifadhi hizo kuona.

Fursa za Nchi Tatu Katika Pori la Ibanda

Katika Pori la Akiba la Ibanda Wilayani Kyerwa kuna eneo ambalo ni mipaka ya nchi tatu za Afrika Mashariki ambapo kwa upande wa Tanzania eneo hilo la pori la akiba linajulikana kama Kagaga, Nchi ya Uganda eneo hilo linaitwa Sophia au “Mirama Hill” na Upande wa Rwanda panaitwa Kajitumba. Eneo hili linatenganishwa na Mto Kagera na Mtalii anapata fursa ya kuona mipaka ya nchi tatu kwa wakati mmoja.

Mara baada ya kutembelea eneo hilo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Gaguti alitoa wito kwa wawekezaji kuona fursa hiyo ikiwa ni pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kujenga Hoteli na vituo vya Utalii ili kutoa fursa kwa Watalii kutoka nchi za Rwanda na Uganda kuingia katika Hifadhi ya Taifa tarajiwa ya Ibanda kupitia mipaka hiyo kwa kuvuka mto Kagera na kuingia katika Hifadhi bila kupita Mipaka ya Mulongo na Rusumo.

“Hapa tukipata wawekezaji tunatakiwa kujenga Hoteli za kisasa, vituo vya utalii ili kama mtalii anataka kutoka Uganda au Rwanda kuja katika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda apite hapa na hakuna ulazima wa kupita Mulongo au Rusumo, hii ni fursa kubwa sana lazima tuitangaze kwa nguvu zote ili tutumie nafasi ya uwepo wa mipaka hii mitatu kupata watalii ambapo tunaweza kujenga vivuko au kupata boti za kitalii za kuwavusa katika Mto huu wa Kagera. Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera 

Wito unatolewa kwa vijana Mkoani Kagera kuanza kuchangamkia fursa kwa kuanza kujiandaa katika masomo ya utalii ambapo watapata ajira za kuongoz Watalii, kujiandaa kusomea uhotelia ili kufanya kazi katika Hoteli za Kitalii zitakazojengwa katika Hifadhi hizo za Taifa Mkoani Kagera, hayo ni pamoja na kusomea lugha mbalimbali ili kupata fursa nzuri ya kuongoza Watalii  kutoka nchi mbalimbali na kuelezea vizuri juu ya maliasili katika hifadhi hizo.

Wawekezaji mbalimbali hasa kwa Mkoa wa Kagera wanatakiwa kuchangamkia fursa hii ya utalii kwa kujenga Hoteli nzuri, hususani katika Halmashauri zetu za Wilaya zinazozunguka Hifadhi hizo tarajiwa za Taifa lakini pia Hoteli hizo kujengwa ndani ya  Hifadhi hizo pamoja na vivutio na vituo mbalimbali vya kitalii ili kuvuti watalii wa ndani na nje ya mkoa kwa ujumla.

Utamaduni, wananchi wanaozunguka katika Hifadhi tarajiwa za Taifa wanakumbushwa kujiandaa kuanzia sasa hasa katika kutengeneza vitu malimbali vya kitamaduni ambavyo vinaweza kuuzwa kwa watalii hasa watakaokuwa wanatoka nchi za nje ili wananchi hawa wajipatie kipato tena kwa fedha za kigeni kupitia vivutio vya kitamaduni vitakavyokuwa vinapatikana katika hifadhi hizo.

Vyakula vya Kitamaduni, Wananchi pia wanatakiwa kuanza sasa kulima kwa wingi vyakula vya kitamaduni kulingana na utamaduni wao na kujiandaa kwa ajili ya kupata soko la vayakula hivyo vinavyopendelewa sana na Watalii na kuona ni namna gani vyakula hivyo vinapikwaje au vinaandaliwaje kitamaduni na ikumbukwe kuwa hiyo  ni mmojawapo ya utalii.

Hoteli kubwa zitahitaji vyakula hivyo kwa wingi kwa maana hiyo wakulima Mkoani Kagera hasa ambako kila zao linakubalika vizuri kulimwa na kustawi wanatakiwa kuiona fursa hiyo mapema ili masoko ya mazao hayo yasije kutekwa na wakulina na wafanyabiashara kutoka mikoa jirani au pengine nchi jirani wakati fursa hiyo ingeweza kuchukuliwa na wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Changamoto 

Chanagamoto kubwa ambayo bado hasa inaikumba Hifadhi ya taifa Tarajiwa ya Ibanda Wilayani Kyerwa ni pamoja na nchi jirani zinazopakana na hifadhi hiyo kujenga Kambi ya Wakimbizi ambayo ipo karibu sana na hifadhi hiyo jambo ambalo linapelekea wakimbizi hao kuvuka mto Kagera na kufuata mahitaji muhimu upande wa pili kama kuni na kuua wanyama pori kwa ajili ya kupata kitoweo au chakula.

Pia nchi jirani zinazopakana na Hifadhi za taifa tarajiwa Mkoani Kagera zimeruhusu makazi ya wananchi kupakana na hifadhi hizo jambo ambalo linachochea ujangiri katika hifadhi pale wananchi wa nchi hizo wanapovuka na kutaka kuendesha shughuli za uwindaji kwenye hifadhi.

Mwisho bado wananchi hasa katika Mkoa wetu wa Kagera hawajachangamkia fursa ya kuwekeza katika Hifadhi hizo na kutoa nafasi kwa wawekezaji kutoka nje ambapo hapo baadae wananchi hawa wa kagera wanaweza kuanzisha migogoro kwa kutokuona manufaa ya hifadhi za taifa tarajiwa kwao. Ni muhimu sana wananchi wazawa kuanza kuchangamkia fursa hizi mara moja ili kujiongezea kipato. Karibu TANAPA Kagera, Karibu Tutalii Kagera.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa