- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali Mkoani Kagera yajipanga vyema kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 haukwamishwi kwa kikwazo chochote hasa maandalizi muhimu ambapo Wasimamizi wa Uchaguzi huo Katika ngazi za Halmashauri za Wilaya nane wameapishwa na kula viapo kusimamia uchaguzi huo.
Wasimamizi hao nane walioteuliwa rasmi Septemba 11, 2019 na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo na wakila viapo vya uaminifu, utii na uadilifu mbele ya Mhe. Flora Kaijage Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Bukoba Septemba 12, 2019 na kuwa wasimamizi rasmi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa Mkoa Kagera.
Kabla ya viapo hivyo Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera Wakili Jovini Rutahinurwa aliwakumbusha wasimamizi wateule kuwa viapo hivyo vipo kwa mujibu wa kanuni za sheria ya uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi za Vijiji, Vitongoji na Mitaa ya mwaka 2019
Kanuni hizo alizitaja Wakili Jovini kuwa ya kwanza ni Kifungu namba 44 kifungu kidogo cha 4 tangazo la Serikali namba 371 la mwaka 2019. Pili, Kifungu namba 46 kifungu kidogo cha 4 tangazo la Serikali namba 372 la mwaka 2019.Tatu, Kifungu namba 47 kifungu kidogo cha 4 tangazo la Serikali namba 373 la mwaka 2019. Nne, Kifungu namba 47 kifungu kidogo cha 4 tangazo la Serikali namba 374 la mwaka 2019 pamoja na Sheria ya Viapo na Matamko ya Kisheria sura ya 34.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora mara baada ya wasimamizi hao kula viapo vyao mbele ya Mhe. Flora Kaijage Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Bukoba aliwapongeza na kuwakumbusha wajibu wao kuwa wameaminiwa na Serikali kwa kupitia mchujo mkali kwahiyo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa utii, uaminifu na uadilifu mkubwa kama walivyoapa.
Profesa Kamuzora aliwataka wasimamizi hao kusoma nyaraka na miongozo yote kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuyaelewa maeneo yao ya utawala ili kuhakikisha hakuna mapingamizi yanayoweza kujitokeza. Pia alisistiza kuwa Serikali kuanzia ngazi ya wizara hado mkoa imefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa ufanisi mkubwa ukilinganisha na uchaguzi wa miaka iliyopita.
Aidha, Profesa Kamuzora alitoa angalizo kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhakikisha wanatoa wagombea wenye sifa hasa katika Wilaya za mipakani za Missenyi, Karagwe, Kyerwa na Ngara kuepusha wahamiaji haramu kugombea nafasi hizo. “Kama ikibainika Serikali itachukua hatua za kisheria kwa wahusika lakini rai yangu ni kwa wananchi kutoa taarifaau pingamizi pale mhamiaji haramu atakapopitishwa kugombea itakapotokea.” Alisisitiza Profesa Kamuzora
Katika hatua nyingine Profesa Kamuzora alisema kuwa Mkoa wa Kagera unatarajia kuadikisha wapiga kura wapatao 1,288,370 na vituo vya kupigia kura vikiwa ni 3,738 kwenye vijiji 662 na Vitongoji 3,665 katika Kata 92 aidha, zikiwa Tarafa 27.
Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoani Kagera walioteuliwa na kuapishwa rasmi Septemba 12, 2019 ni Bw. Richard Masanilo Mihayo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Bablyus Lubingo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Bw. Albert Mamimo Msemwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bw. Rajab Khasim Byoma Halmashauri ya Wilaya Karagwe.
Wengine ni Bw. John Mayuga Msafiri Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Bw. Lucas Haga Daudi Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Bw. Costantino Francis Msemwa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo na Bi Essery Felician Pima Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa