• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Wawekezaji Kutoka Nchi Jirani Sasa Wapishana Kuchangamkia Uwekezaji Kagera ni Baada ya Wiki ya Uwekezaji Kuwaonesha Fursa

Imewekwa : September 11th, 2019

Juhudi za viongozi wa mkoa wa Kagera kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha uchumi wa nchi za Afrika Mashariki na Kati zilizoanzia katika Wiki ya Uwekezaji Kagera sasa zaanza kuzaa matunda ni baada ya kundi la wawekezaji kutoka nchi jirani ya Rwanda kuitikia wito wa kuwekeza mkoani humo.

Kundi la Wawekezaji kumi wanaomiliki mampuni mbalimbali ya biashara nchini Rwanda walioamua kuunda Kampuni moja ya uwekezaji mkoani Kagera katika Sekta ya ufugaji wa kisasa na kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama waliwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ili kumweleza nia yao na kuwa wapo tayari kuwekeza katika ufugaji na kiwanda cha kusindika nyama.

Bw. William Kawamala kiongozi wa wawekezaji hao kumi kutoka nchini Rwanda alimweleza Mkuu wa Mkoa Gaguti kuwa wapo tayari kuwekeza katika sekta ya ufugaji  wa kisasa wa ng’ombe katika Kampuni za  Ranchi za Taifa (NARCO) baada ya kupata fursa hiyo katika Wiki ya Uwekezaji Kagera iliyofanyika tarehe 12 hadi 17 Agosti, 2019.

“Sisi baada ya kushiriki Wiki ya Uwekezaji Kagera tulivutiwa kuwekeza katika Sekta ya ufugaji, na tuliporudi kwetu nchini Rwanda tilikaa pamoja na kukubaliana tujiunge kwa pamoja wafanyabiashara kumi ili kuanza uwekezaji mara moja, ndiyo maana tupo hapa ili kuanza hatua za awali pia tumekuja kuona maeneo ya kufugia na kuweka kiwanda..”  Alifafanua Bw. Kawamala

Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwakaribisha wawekezaji hao na kusema kuwa mkoa upo tayari kuwapa ushirikiano,  hatua ya kwanza alimwelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NARCO Prof. Philemon Wambula pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Sekretarieti ya mkoa  kuwaonesha maeneo yaliyotengwa ili wakubaliane nayo na taratibu  za kusajili kampuni na kuanza uwekezaji zianze mara moja.

“Baada ya Wiki ya Uwekezaji mwitikio umekuwa mkubwa sana wa wawekezaji kuja kwetu kuchangamkia fursa zilizopo Kagera na sisi tumejipanga tunawapokea na kuwaelekeza taratibu za uwekezaji, lakini jukumu letu ni kuhakikisha fursa zote ambazo wawekezaji wameziona wanazitumia katika uwekezaji ili kukuza uchumi wa mkoa wetu.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Profesa Philemon Wambula Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni za Ranchi za Taifa (NARCO) alisema kuwa mkoa wa Kagera bado una fursa kubwa za uwekezaji katika sekta ya mifugo hasa katika viwanda vya kusindika nyama na maziwa pia uwekezaji katika malisho ya mifugo aidha, NARCO bado inayo maeneo makubwa ya kuwekeza.

Wawekezaji hao kumi walieleza kuwa baada ya kuona maeneo wanataka kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe, ujenzi wa kiwanda cha kuchinja na kusindika nyama kwa viwango vya kimataifa. “Kwasasa baadhi ya Hoteli kubwa nchini Rwanda zimeanza kuagiza nyama kutoka nchi za Ulaya wakati tukifuga kisasa hapa Kagera tunaweza kuilisha Rwanda.”  Walisisitiza Wawekezaji hao kutoka nchini Rwanda.

 

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa