• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Kijuu (Kulia) Akikagua Stoo ya Dawa Rubale Halmashauri ya Wilaya Bukoba

Imewekwa : September 14th, 2017

Wazee Mkoani Kagera Wanufaika Na Vitambulisho Vya Kupatiwa Huduma Za Afya Bure Na Mapambano Dhidi Ya Malaria Yaendelea

Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu afanya ziara ya kukagua huduma za afya Mkoani Kagera na kuzindua unyunyiziaji wa dawa ya kuua viluilui katika mazalia ya mbu ili kupunguza tatizo la malaria mkoani hapa.

Ziara hiyo iliyoanza tarehe 12 Septemba, 2017 katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba  Mhe. Kijuu alizindua ugawaji wa vitambulisho vya kupata huduma ya afya kwa wazee ili watibiwe katika vituo vya afya bure bila malipo yoyote.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alilenga kukagua na kujihakikishia uwepo wa dawa katika vituo mbalimbali vya afya kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Pili alilenga kuhamasisha wananchi kujikinga na kuchukua hatua za kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo katika Mkoa wa Kagera.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alilenga kuhamasisha vituo vyote vya afya kutumia mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielekitroniki ili kuongeza mapato yatayoboresha huduma kwa wananchi. Katika ziara hiyo Mhe. Kijuu alijihakikishia kuwa dawa zipo za kutosha kwenye vituo na kutoa rai kwa wananchi kufika katika vituo hivyo pindi wanapohisi wanaumwa ili kupatiwa huduma za matibabu.

Katika ziara hiyo Mhe. Kijuu aliwasistiza watendaji wa Halmashaui za Wilaya kuhakikisha wazee wanapatiwa vitambulisho na kusema kuwa wazee hao wakati wa ujana wao walizalisha na kulitumikia taifa kwa nguvu zao zote na sasa ni wakati wao kuhudumiwa hasa kupatiwa huduma za afya bure bila kutozwa fedha zozote.

Aidha, Mhe. Kijuu alimpongeza Rais John Pombe Magufuli ambaye naiongoza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwakumbuka wazee na kuwapatia vitambulisho ambavyo vitawaruhusu wazee wa Tanzania kupatiwa huduma za afya bure bila malipo.

Katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba tayari wazee 900 wametambuliwa na kupewa vitambulisho, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi tayari wazee 1500 wametambuliwa na wanatarajiwa kupatiwa vitambulisho na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Zaidi ya Wazee 200 tayari wamepatiwa vitambulisho vya kupatiwa huduma ya afya bure.

Agizo ni kuwa Halmashauri zote zinatakiwa kuwatambua wazee na kuwapatia vitambulisho hivyo. Aidha Mhe. Kijuu aliziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinanyunyizia dawa ya kuua viluilui katika madimbwi, kandokando ya mito ili kuharibu mazalia ya mbu, pia kuhakikisha Halmashauri zote zenye shehena ya dawa katika maghara ya dawa, dawa hizo zisambazwe  vituoni ili kutoa huduma kwa wananchi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dk. Thomas Rutachunzibwa katika ziara hizo alitoa rai kwa watendaji  wa Halmashauri kuona umuhimu wa kufunga mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielekitroniki ili kuongeza mapato katika vituo hivyo jambo ambalo litaboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kuacha utegemezi na vituo kujiendesha vyenyewe kwa makusanyo yao wenyewe.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alitembelea vituo vya afya Rubale Wilayani Bukoba, Buyango na Bunazi Wilayani Missenyi, pia na Kituo cha Afya Zamzam Manispaa ya Bukoba. Vilevile alitembelea maeneo dawa ya kuua viluilui inakonyunyiziwa hasa katika madimbwi na maji yaliyotuhama.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa