- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera Kuibua Vipaji Kupitia Michezo ya Umiseta Mwaka 2018
Na Sylvester Rapahel
Mkoa wa Kagera tayari umeanza maandalizi ya kuibua vipaji vipya vya wanafunzi wa shule za Sekondari katika mashindano ya UMISETA ambayo hukutanisha wanafunzi wanamichezo kutoka katika Halmashauri zote za Wilaya na kuunda timu moja ya mkoa kwaajili ya kushiriki mashindano ya UMISETA Kitaifa.
Mkoa wa Kagera ni mkoa unaoaminika kuzalisha vipaji vingi hasa katika michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, michezo ya riadha na mchezo wa ngumi pamoja na michezo mingineyo mingi. Kwa mwaka huu 2018 mkoa umejipanga kuhakikisha unatoa ushindani mkubwa katika mashindano ya UMISETA Kitaifa kwa kupeleka timu yenye uwezo na yenye vipaji vyakutosha Jijini Mwanza.
Kutokana na juhudi zinazoendelea kufanyika ili kuhakikisha michezo inarejea katika enzi zake Mkoani Kagera, Serikali kupitia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe iliupa heshima Mkoa wa Kagera kuwa mkoa mmojawapo kati mikoa mitano kufanya uzinduzi wa michezo ya UMISETA Kitaifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca Cola.
Akiwa katika uzinduzi huo Waziri Mwakyembe Mkoani Kagera Mei 12, 2018 alisema kuwa Mkoa wa Kagera unategemewa sana na Taifa kutoa vipaji vingi kupitia michezo ya UMISETA hasa katika timu ya Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys kwani Kagera kuna wachezaji wengi wenye vipaji binafsi.
“Nakumbuka sana miaka ya nyuma kidogo Mkoa wa Kagera ulikuwa tishio sana katika mambo ya michezo na tunataka kiukweli mkoa huu uwe hazina yetu ya wachezaji katika michezo yote na ndiyo maana tumeamua kuja kufanya uzinduzi wa UMISETA hapa na kuhamasisha vijana kuonesha vipaji vyao ili wapate ajira kupitia michezo,” Alifafanua Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe pia alisema baada ya Shirikisho la Mpira nchini kukaa vizuri kwa sasa Shirikisho la Mpira Duniani FIFA limekubali kutoa tena fedha za kukarabati viwanja vya michezo nchini baada ya kusitisha kutoa fedha hizo kutoakana na kutumika vibaya. Aidha, Waziri alisema kuwa Mkoa wa Kagera atauangalia kwa jicho la karibu sana katika mgao wa fedha hizo ili viwanja vya Kagera vikarabatiwe kuibua vipaji.
Naye Afisa Michezo Mkoa wa Kagera Bw. Kepha Elias akiwa Chuoni cha Ualimu Katoke kwenye kambi ya mkoa ya mashindano ya michezo ya UMISETA alisema kuwa mwaka huu 2018 mkoa wa Kagera lazima uibuke na ushindi kitaifa na kuibua vipaji vingi kwani mfumo wa kupata vipaji hivyo ni mzuri sana ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa