• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Waziri Jaffo Apongeza Ushirikiano wa Wananchi wa Nyakazi Biharamulo Katika Kutekeleza Miradi ya Maendeleo

Imewekwa : August 10th, 2018

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jaffo awapongeza wananchi wa Kata ya Nyakanazi Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera kwa ushirikiano wao wa kuchangia na kushiriki katika kutekeleza miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa Kituo cha Afya Nyakanazi ambacho kimekamilika ujenzi wake baada ya Seriakli kutoa Shilingi milioni 500 ili kiweze kuboreshwa na kutoa huduma muhimu za afya kwa wananchi.

Waziri Jaffo aliyasema hayo Agosti 9, 2018 alipofanya ziara ya siku moja na kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho ambapo alisema kuwa amaeridhishwa na ujenzi ulivyofanyika kuwa ni kiwango kinachoridhisha na thamani ya fedha iliyotolewa inaonekana katika majengo yaliyojengwa na mengine kukarabaitiwa.

“Nawapongeza wananchi wa Kata ya Nyakanazi kwa kujitoa kushirikiana na Serikali kuhakikisha kituo hiki cha Nyakanazi kinajengwa na kukamilika, nyinyi wananchi mmekuwa mstari wa mbele kutekeleza wajibu wenu pale mlipotakiwa kufanya hivyo na ndiyo maana kituo chenu kimekalika.” Alifafanua Waziri Jaffo.

Waziri Jaffo alizidi kusisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wananpata huduma bora hasa akinamama wajawazito katika suala la upasuaji wakati wa kujifungua sasa tatizo hilo limefika mwisho baada ya kituo hicho kukamilika. Aidha, Waziri Jaffo aliongeza kuwa Serikali baada ya kuridhishwa na ujenzi ulivyotekelezwa katika kituo hicho imetoa tena shilingi milioni 400 nyingine za kujenga kituo kingine katika Halmashauri ya Wilaya Hiyo ya Biharamulo.

Pamoja na kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Waziri Jaffo alitoa tahadhari kwa Halmashauri hiyo kusimamia mapato ambapo alisema Biharamulo haifanyi vizuri katika kukusanya mapato. Pia aliagiza kuitishwa kwa Balaza Maalum la Madiwani ili kujadili ripoti ya Tume ya uchunguzi ilioundwa kuchunguza mapato yanavuja wapi na kama ikigundulika kuna watumishi waliohusika wachukuliwe hatua mara moja naye apewe taarifa.

Kituo cha Nyakanazi kimekamilika ujenzi wake kwa jumla ya shilingi milioni 700 ikiwa shilingi milioni 500 zilitolewa na Serikali kujenga majengo ya Wodi ya akinamama na watoto, Wodi ya watoto, chumba cha kuhifadhi maiti, Nyumbambili (Two in one) za watumishi na kukarabati chumba cha upasuaji. Pia shilingi milioni 200 zilitumika kununua vifaa katika kituo hicho.

Waziri Jaffo alimaliza kwa kusema kuwa Serikali itajenga vituo vyote vya afya Wilayani Biharamulo ili wananchi wote wapate huduma safi, pia alisema wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 115 tu lakini hadi sasa vimejengwa vituo 210 na tayari vituo 97 vimepewa fedha kujengwa, hayo ni mafanikio na mapinduzi makubwa katika Sekta ya Afya.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa