- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Selemani Jafo aridhishwa na utendaji kazi wa viongozi wa Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri Jafo ameyasema hayo akiwa Mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba katika ziara ya siku moja Juni 5, 2020 wakati akitembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Shule za Sekondari za Rugambwa (wasichana) na shule ya Sekondari ya Ihungo (Wavulana) pia na mradi wa barabara za kilometa tano wenye gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.3.
Akiwa katika Shuleza Sekondari Ihungo na Rugambwa Waziri Jafo alisema kuwa ameridhishwa sana na ukarabati wa shule hizo kongwe ulivyofanyika na kuzifanya shule hizo kuwa mpya kabisa. Pia aliwashukuru wanafunzi wa kidato cha sita katika shule hizo kutii maelekezo ya Serikali baada ya janga la ugonjwa wa KORONA kwa kurudi shule kwa asilimia 99 kuendelea na masomo yao.
Waziri Jafo aliwapongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Ihungo kwa viwango vya hali ya juu sana ambapo alisema kuwa ubora wa majengo ya shule hiyo ni wa kwanza nchini na kutoa rai kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera kuacha ndoto za kugeuza shule hiyo kuwa Chuo Kikuu badala yake wanafunzi wasome katika mazingira bora zaidi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera akitoa taaarifa katika shule hizo alisema kuwa Mkoa wa Kagera unazo shule za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita 36 zenye wanafunzi wa kidato cha sita 3,590 na wanafunzi 3,393 tayari wameripoti katika shule hizo kuendelea na masomo yao ya kidato cha sita wanafunzi 197 asilimia 5 bado hawajaripoti.
Ikumbukwe kuwa Serikali ilitoa zaidi ya shilingi milioni 872 kwaajili ya ukarabati wa shule ya Sekondari Rugambwa na zaidi ya shilingi bilioni 11 kuijenga upya shule ya Sekondari Ihungo baada ya Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016 na kufanya uharibifu wa miundombinu yote ya Shule hiyo na kulazimika kujengwa upya.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo alitembelea na kukagua mradi wa barabara za kilometa (5) tano katika Manispaa taya Bukoba ambapo hakuridhishwa na utekelezaji wa barabara hizo kwa kusuasua na kutumia muda mrefu kukamilika ujenzi wake ambapo alitoa maagizo kwa Mkandarasi JASCO ROAD CONSTRUCTION kuhakikisha anakamilisha kazi ya barabara zote ifikapo Juni 15, 2020 vingnevyo asipokamilisha barabara hizo hatopewa tena kazi yoyote katika Wizara yake ya TAMISEMI.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa