- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mpina Amsimamisha Kazi Mtumishi Aliyeruhusu Samaki Kutoroshewa Nchini Burundi Bila Kufuata Sheria Za Nchi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amtumbua Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi mpakani Bw. Ayoub Ngoma ambaye aliruhusu gari lililokuwa limebeba samaki wasioruhusiwa kuvuliwa zaidi ya tani mbili ambapo samaki hao walikuwa wakitoroshwa kuelekea nchini Burundi kupitia mpaka wa Murusagamba Wilayani Ngara.
Waziri Mpina alimwagiza Katibu mkuu wa Wizara yake Dk. Yohana Budeba kuhakikisha anamsimamisha kazi mara moja mtumishi huyo kabla ya saa 6:00 mchana na kupewa taarifa pia na taratibu za kumfukuza kazi zianze mara moja baada ya kuonekana anashirikiana na waharifu kuihujumu Serikali.
Agizo hilo lilitolewa na Waziri Mpina akiwa katika siku yake ya pili ziarani Mkoani Kagera tarehe 6.12.2017 alipofanya ziara katika Idara ya Maendeleao ya Uvuvi Mkoa wa Kagera na kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu Afisa Mfawidhi Usimamizi wa Raslimali zaUvuvi Kagera Bw. Gabriel Mgeni ambapo alitolea taarifa tukio hilo lililotokea Murusagamba Wilayani Ngara Desemba 3, 2017.
Bw. Mgeni alisema kuwa tarehe 3.12.2017 majira ya saa 9:00 asubuhi Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara walikamata gari lenye namba za usajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter ikiwa imepakia samaki wenye uzito wa zaidi ya kilo 2,000 aina ya Sangara kilo 530 Samaki aina ya Sato.
Kwa mujibu wa sheria namba 22 ya mwaka 2003 watuhumiwa waliokamatwa wanasafirisha samaki hao walikuwa wamekiuka taratibu zifuatazo ; kuvua samaki wenye ukubwa zaidi ya sentimita 85 na wadogo chini ya sentimita 50, kutokuwa na kibali cha kusafirisha mazao ya uvuvi, kutolipa mrahaba wa Serikali, kutokuwa na cheti cha afya pamoja na leseni ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi.
Bw. Mgeni alisema kuwa samaki hao baada ya kukamatwa Mahakama ilitoa kibali maalum na kugawa samaki hao kwenye taasisi za Serikali na wananchi. Waziri Mpina alizishukuru Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera kwa juhudi kubwa za kupambana na vitendo haramu vya kutorosha maliasili za nchi nje ya nchi.
Waziri Mpina pia alitoa rai kwa watumishi ambao wapo chini ya Mamlaka yake kuwa kwa yeyote ambaye atagundulika kujihusisha na vitendo vya kuihujumu Serikali hawezi kubaki kazini kwani akibainika tu lazima achukuliwe hatua kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi moja kwa moja. Vilevile alimwagiza Mwanasheria wa Wizara yake kuhakikisha anaharakisha mchakato wa kuitaifisha gari lililokamatwa na samaki likiekea nchini Burundi.
Aidha, katika hatua nyingine Waziri Mpina alijionea mafurushi 6 ya samaki aina ya migebuka kilo 240 yaliyokamatwa katika kituo Kikuu cha Mabasi Bukoba yakisafirishwa kwenda nchini Uganda, Mabondo kilo 100 ambapo mtuhumiwa wake alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi, Majora 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20 na mitumbwi zaidi ya 50 iliyokamtwa katika doria .
Waziri mpina aliiagiza Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Kagera kuhakikisha inaendelea na juhudi za kukamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu na utoroshaji wa samki nje ya nchi ambapo tani 100 hutoroshwa kila wiki kuelekea nchi jirani. Waziri Mpina amehitisha Ziara yake ya Siku mbili Mkoani Kagera leo tarehe 6.12.2017 na kuelekea Mkoani Kigoma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa