- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mpina Amutimua Mwekezaji Mbabaishaji Agri Ranch Katika Ranchi ya Taifa ya Kagoma Mkoani Kagera
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ampa siku saba mwekezaji wa Ranchi za Kagoma, Mabale na Kikurula AGRI RANCHI kuwa ameondoa mifugo yake katika Ranchi hizo baada ya kukiuka masharti ya mkataba wake na Kampuni ya Huria (Ranchi) za Taifa (NARCO) na kuendelea kutumia Ranchi hizo kwa miaka mitano bila kutimiza masharti ya Mkataba.
Waziri Mpina akiwa Mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 5 hadi 6 Desemba 2017 alitembelea Huria (Ranchi) ya Kagoma Wilayani Muleba na kukutana na Mwekezaji AGRI RANCH ambaye anawekeza katika Ranchi tatu za Kagoma, Mabale na Kikurula na kutembelea mifugo yake, kukagua miundombinu aliyowekeza katika Ranchi ya Kagoma pia na Kuongea na mwekeza ji huyo.
Baada ya kutembelea miundombinu katika Ranchi hiyo na kupata maelezo ya AGRI RANCH pamoja na Meneja Mkuu wa NARCO Profesa Philemon Wambura Waziri Mpina alitoa uamuzi kuwa anakubaliana na maamuzi ya NARCO ya kuvunja Mkataba na AGRI RANCH kwasababu Kampuni hiyo ilikiuka masharti ya Mkataba huo tangu mwaka 2012 ilipopewa Ranchi hizo tatu kuwekeza.
“Kuanzia sasa nakubaliana na maamuzi ya NARCO ya kuvunja Mkata ba na Kampuni hii kwani wamekiuka Mkataba tangu mwaka 2012 walipopewa Ranchi zetu kuwekeza. katika Mkataba huo AGRI RANCH ilitakiwa kujenga kiwanda cha kusindika nyama na machinjio ya kisasa lakini hadi sasa kwa miaka mitano hawajawahi kufanya lolote ,” alisisitiza Waziri Mpina.
Vilevile Waziri Mpina alisema kuwa AGRI RANCHI ilitakiwa kuilipa Serikali kiasi cha Shilingi bilioni tatu kila mwaka lakini hadi sasa haijawahi kulipa fedha hizo bali wamelipa kiasi kidogo sana katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba , kwahiyo kwa miaka mitano wanadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 15 pia Kampuni hii ilitakiwa kuwa na ng’ombe zaidi 25,000 katika Ranchi zetu lakini hadi sasa ng’ombe waliopo ni 4500 tu.
Aidha, Meneja Mkuu wa NARCO Profesa Philemon Wambura alisema Kampuni ya AGRI RANCH imekiuka mashariti yote ya mkataba na tayari NARCO wameionya mara nyingi kampuni hiyo na kukaa nao kwa majadiliano mara kwa mara laikini AGRI RANCH hawakutekeleza chochote ambapo NARCO ikaamua kuvunja Mkatana kutoa “notice” ya mwekeza huyo kuondkoa tangu mwaka 2014 lakini bado ameendelea kukaidi hadi sasa.
Baada ya maelezo hayo Waziri Mpina alisema kuwa Serikali haiwezi kuendelea kwavumilia wawekezaji waongo ambao hawana mitaji lakini wanaidanganya Serikali na kutumia Raslimali za wananchi isivyopaswa ambapo aliwaagiza NARCO kufanya tathimini ya kina juu ya hasara iliyosababishwa na Kampuni hiyo na kuilipa Serikali ikiwa ni pamoja na Bilioni 15 walizokwepa kulipa awali.
Katika hatua nyingine Waziri Mpina alimwagiza Meneja Mkuu wa NARCO Profesa Philemon Wambura kuhakikisha kuwa ndani ya Siku sana awe amepeleka Meneja Katika Ranchi ya Kagoma na walinzi wa kuilinda Ranchi hiyo isivamiwe wakati mwekezaji anaendelea kuondoa mifugo yake katika Ranchi hiyo.
Pia kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa Vitalu vya ufugaji Mkoani kagera Waziri Mpina alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango kwa kushirikiana na NARCO kubaini mipaka halisi ya vitalu na kutoa mapendekezo juu ya wananchi waliovamia vitalu hivyo ili kuondoa kabisa tatizo la uvamizi wa vitalu vya wawekezaji.
Akijitetea mbele ya Waziri Mpina Meneja wa Kampuni ya AGRI RANCH Bw. Rutagwelela Mbelwa alisema hawakujenga kiwanda cha nyama kutokana na ng’ombe aina ya ankole kutokuwa na nyama inayokidhi viwango kwahiyo kampuni hiyo ilijikita katika ufugaji wa ng’ombe aina ya borani ili kupata nyama inayokidhi viwango vya kimataifa ndipo kiwanda kingejengwa.
Pili Bw. Mbelwa alisema kuwa Kampuni yake AGRI RANCH inaomba kubaki na na Ranchi moja ya Kagoma lakini Mabale na Kikurula Serikari inaweza kuzitaifisha ambapo maelezo hayo hayakubatilisha msimamo wa Waziri Mpina na kusisitiza kuwa waondoe mifugo yao mara moja katika Ranchi za Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa