• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awaasa Wajumbe wa Kamati Kuu CCM Mkoa Kuacha Malumbano na Migogoro Ili Chama Kiisimamie Serikali Kutekeleza Ilani

Imewekwa : February 21st, 2019

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katika siku yake ya pili ziarani Mkoani Kagera afanya kikao na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa na kuongea na wajumbe wa kamati hiyo ambapo amewakumbusha wajibu wao wa kuhakikisha CCM inawafikia wananchi hadi ngazi za chini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mlezi wa CCM mikoa ya Kagera na Kigoma katika kikao cha Kamati Kuu CCM mkoa aliwataka wajumbe kuhakikisha chama hicho kinakuwa mkombozi na kuleta matumaini kwa wananchi  kwa kuisimamia Serikali kutekeleza ilani na kutimiza ahadi zilizohaidiwa na chama hicho mwaka 2015.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mlezi wa CCM mkoa wa Kagera aliwakumbusha Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanawasilisha taarifa za Wilaya zao za utekelezaji wa ilani katika vikao vya Halmashauri Kuu za Wilaya kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera anavyofanya kwa kuwasilisha taarifa ya utekeklezaji wa ilani ya mkoa katika Kikao cha Kamati kuu CCM Mkoa.

Akitoa ufafanuzi juu ya uwasilishwaji wa taarifa hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya wanantakiwa kuandaa taarifa hizo na Wakuu wa Wilaya kuziwasilisha katika Vikao vya Kamati Kuu za Wilaya ili Chama (CCM) ambacho kimeiweka Serikali madarakani kiweze kuisimamia vizuri Serikali yake. Aidha alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kusimamia agizo hilo kwa Wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Kagera.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwataka wajumbe wa Kamati Kuu CCM Mkoa kuacha malumbano na migogoro katika chama badala yake washikamane na kushirikiana kuhakikisha CCM inatekeleza ahadi zake kwa wananchi pia na kuisimamia Serikali kutekeleza ilani katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera.

Vile vile Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaagiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilaya kuhakikisha wasimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kutosha na kushirikiana na Wenyeviti wa Halmashauri zao kutenga fedha za kuchimba visima vya maji vifupi na virefu kwa wananchi ili kumtua mama ndoo kichwani.

“Nitashangaa kama Mkurugenzi atashindwa kusimamia mabilioni ya fedha za miradi ya maji tulizo waletea ili wananchi wake wapate maji, pia nafurahi Wenyeviti wa Halmashauri mpo hapa hebu shirikianeni kukusanya mapato katika Halmashauri zenu na mtenge angalau million 20 kwajili ya kuchimba visima vya maji vifupi wananchi wetu wapate maji.” Alifafanua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaeleza wajumbe wa Kamati Kuu CCM Mkoa kuwa Kamati Kuu CCM taifa ilimwagiza kutilia mkazo kwenye kilimo hasa kilimo cha kahawa Kagera ambapo alisema kuwa anazo taarifa kuwa Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani humo baadhi vimelipa malipo ya pili na vingine bado vinaendelea kukamilisha huku vikijiandaa na msimu mpya.

“Zao la kahawa ni zao pendwa Mkoani Kagera wahimizeni wananchi waendelee kulima kwa nguvu zao hili lakini pia sisi wajibu wetu ni kuimalisha kilimo hiki na nawaagiza viongozi kujipanga na msimu mpya ujao ili tusije kuingia katika matatizo yaliyotokea msimu uliopita.”  Aliagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Mwisho Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwataka wajumbe wa Kamati Kuu CCM Mkoa wa Kagera kulinda mali za chama na kuacha kugombania mapato yanayotokana na baadi ya vitega uchumi vya chama hicho kwani wote wanajenga nyumba moja.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa