• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi (Kushoto) Akisaini Kitabu Katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.

Imewekwa : February 19th, 2018

Waziri Lukuvi Asema Migogoro ya Ardhi Imepungua Kagera Asema Serikali Imejipanga Kukomesha Ujenzi Holela

Serikali katika Mkao wa Kagera yapunguza migogoro ya ardhi kwa kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu Tano changamoto kubwa iliyobaki ni kupangilia miji na kuzuia ujenzi holela katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba.

Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2018 na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Wiliamu Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne katika Wilaya za Bukoba (Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoa), Karagwe, Kyerwa na Ngara.

Mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa ihusuyo Wizara yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Waziri Lukuvi aliwapongeza watendaji katika mkoa kuendelea kutatua migogoro ya ardhi na kutozalisha migogoro mipya bali migogoro iliyopo ni ile iliyozalishwa kipindi cha nyuma kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano haijaingia madarakani.

Waziri Lukuvi alisema kuwa Serikali iliamua kurasimisha maeneo ambayo tayari yalikuwa yamejengwa holela ili kupangilia miji lakini kuanzia sasa wananchi hawaruhusiwi kujenga holela na Watendaji wa Halmashauri hasa Maafisa wa Mipango Miji wanatakiwa kutoa Ramani za kila eneo kwa Watendaji wa Mitaa ili kuzuia ujengaji holela bila vibali vya ujezni vya Halmashauri husika.

“Kulikuwa na ucheleweshaji wa vibali vya ujenzi katika Halmashauri lakini kwa sasa Serikali imeamua kutoa kipengele cha vibali kupitishwa na Mabaraza ya Madiwani ili kuharakisha vibali vya ujenzi kutoka haraka kwa mwananchi anayetaka kujenga nyumba yake,” Alisistiza Waziri Lukuvi.

Katika kusisitiza suala hilo Waziri Lukuvi alisema kuwa Wataalamu wa Ujenzi, Mipango Miji na Mkurugenzi wanatakiwa kukaa na kupitia maombi ya vibali vya ujenzi na kutoa taarifa katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani. Waziri Lukuvi alisema kuwa tayari Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI amesaini waraka wa kuondoa kifungu hicho ili vibali vipitishwe na Wataalam.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi alitoa rai kwa wananchi wa Kagera kuwa kuna wananchi mashamba yao yapo katika miji lakini hawataki yapimwe ambapo alitoa karipio kali kwa wananchi hao na kusema kuwa mpangaji wa ardhi ni Halmashauri, kama Serikali ikihitaji ardhi hiyo itamfidia mwananchi husika na kutumia ardhi hiyo kama ilivyopangwa.

Pamoja na kutatua migogoro ya ardhi iliyoshindikana katikaHalmashauri za Wilaya zilizotajwa hapo juu Waziri Lukuvi pia atafuatilia suala la ulipaji wa kodi za ardhi katika maeneo atakayotembelea ili kona jinsi kodi hizo zinavyokusanywa na kuwahamasisha wananchi kulipa kodi hizo na Halmashauri kuchukua wajibu kikamilifu katika ukusanyaji.

Ikumbukwe kuwa katika Mkoa wa Kagera vimepimwa viwanja 2,897 kuanzia mwaka 2016 hadi kufikia sasa, aidha Halmashauri za Wilaya zote nane katika Mkoa wa Kagera zinaendelea na upimaji na kutao hati za viwanja.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa