- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
World Vision Kagera Waonesha Mfano Wamuunga Mkono Mkuu Wa Mkoa wa Kagera Katika Kampeini Yake ya Kupanda Miti ya Matunda
Shirika lisilo kuwa la Serikali World Vision Tanzania Kanda ya Kagera limemuunga Mkono Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Kampeini yake ya kupanda miti ya matunda katika Mkoa wa Kagera ili kuondoa tatizo la udaumavu, utapiamulo na kwashakoo kwa wananchi wa Kagera hasa watoto.
Shirika la World Vision Kanda ya Kagera limeto kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Miche 200 ya miti ya matunda aina mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 2,000,000/= na Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliikabidhi miche hiyo kwa Taasisi za Shule katika Manispaa ya Bukoba ili ikapandwe kwenye mazingira ya Taasisi hizo.
Akikabidhi miche ya matunda Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Kagera Bibi Juliana Charles alisema wameamua kummunga mkono Mkuu wa Mkoa katika juhudi zake za kuhakikisha miti ya matunda inapandwa na matunda yanapatikana kwa wingi ili kuhamasisha wananchi kula matunda na kupunguza udumavu, utapiamulo na kwashakoo hasa kwa watoto.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea miche hiyo alilishukuru shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Kagera kwa kutoa misaada ya mara kwa mara na kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kuondoa umasikini na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.
“World Vision wamekuwa wa msaada kwa Mkoa wetu wa Kagera, nakumbuka wakati wa Tetemeko Shirika hili lilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha hali za wananchi zinarejeshwa haraka sana, pia kampeini hii niliizindua tarehe 26 Januari, 2018 lakini unaweza kuona sasa tayari wameitikia wito na kuniunga mkono nawashukuru sana,” Alishukuru Mhe. Kijuu
Aidha, Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alitoa wito kwa Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali kumuunga mkono katika kampeini ya kupanda miti ya matunda ambapo alisema kuwa miche ya miti ya matunda ina gharama kubwa kidogo kwani kila mche mmoja unauzwa kwa gharama ya shilingi 10,000/= jambo ambalo mwananchi wa kawaida yawezekana asimudu gharama ya kununua lakini Taasisi zikijitolea wananchi wanaweza kugawiwa miche hiyo bure na wakaipanda.
Tayari Mkuu wa Mkoa ameagiza kila mwananchi kupanda miche mitano ya matunda katika eneo lake pia na Taasisi zote zihakikishe zinapanda miche ya matunda katika maeneo yao. World Vision Tanzania Kanda ya Kagera wamekabidhi miche ya matunda 200 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Februari 26, 2018
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa