• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Ziara ya Rais Magufuli Mkoani Kagera Yatoa Mwangaza na Njia ya Kukuza Uchumi wa Mkoa na Taifa la Tanzania

Imewekwa : January 23rd, 2021

Mkoa wa Kagera wafungua fursa za maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Tano ya Serikali inayoongozwa na  Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni baada ya kuwa mkoa wa kwanza  nchini kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika ziara ya kikazi tangu uchaguzi mkuu kukamilika  Oktoba 28, 2020.

Ziara ya kikazi ya siku mbili (Januari 18 hadi 19, 2021) ya Rais Magufuli  imeuacha Mkoa wa Kagera katika hali ya matamanio ya  wananchi wake kuendelea kuchapa kazi ili kuifikisha Kagera kwenye ngazi ya juu ya kiuchumi na hayo yanatokana na kusikia na kuona kwa macho nini Serikali ya Awamu ya Tano inafanya, na inatarajia kufanya nini ili Kagera ipae kiuchumi.

Rais Magufuli Kutelea Nini Kagera?

Katika ziara yake Mkoani hapa Rais Magufuli alizindua shule ya Sekondari Ihungo  ambayo imejengwa upya na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 10.9 baada ya majengo ya shule hiyo kuharibiwa kwa kiwango kikubwa na Tetemeko la Ardhi  Septemba 10, 2016 sasa shule hiyo yenye majengo yenye viwango vya hadhi  ya  Chuo Kikuu inahudumia wanafunzi kutoka Kagera na nchi nzima.

Pili, Rais Magufuli aliweka jiwe la Msingi katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kagera kinachojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 22. Chuo hicho kikamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wa kozi ndefu 800 na kozi fupi za ufundi stadi 1600 jumla ya  wanafunzi 2400 kwa mwaka.

Hii ni fursa kubwa ya kiuchumi ukiachana na Ujenzi wa Chuo hicho cha Ufundi Stadi VETA Kagera lakini manufaa kwa wananchi wa Kijiji cha Burugo pale kinapojengwa chuo hicho watanufaika kiuchumi kutokana mwingiliano mkubwa wa watu, tayari Rais Magufuli ameagiza wananchi hao wapatiwe huduma za maji, umeme, na kupimiwa ardhi zao. Ajira tayari wananufaika  nazo katika ujenzi unaoendelea katika eneo lao.

Tatu, kutokana na madini ya nickel kuwa na uhitaji mkubwa  duniani kwa sasa na madini hayo yenye kiwango cha ubora duniani yanapatikana mkoani Kagera  Kabanga Wilayani Ngara, Rais Magufuli aliona ni muhimu mkataba wa uchimbaji wa madini hayo wenye thamani ya Dolla za Kimarekani Milioni 664 sawa na Shilingi Trioni 1.5 ambayo  utafiti wake ulianza mwaka 1976 usainiwe ndani ya mkoa wa Kagera Bukoba  kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED.

Pamoja na kuwa Taifa la Tanzania litanufaika na uchimbaji wa  madini ya Nickel lakini kipaumbele cha Serikali ni kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera hasa wanaopakana na mgodi wa Kabanga Nickel Wilayani Ngara ambao watapata manufaa mengi  ikiwemo ajira katika mgodi huo,  tenda mbalimbali, uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali vitapata soko aidha, Rasi Magufuli aliwasisitiza wananchi hao kuzalisha chakula kwa wingi kwani neema inakuja.

Nne, Katika kuhakikisha wafugaji wanapata soko la maziwa wanayoyazalisha kutokana na mifugo yao Rais Maguli aliweka jiwe la msingi katika Kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo chenye thamani ya shilingi bilioni 8.9  Kiyanga Wilayani Karagwe ambapo kiwanda hicho kikikamilika kitakawa na uwezo kusindika lita 10,000 za maziwa kwa siku na tani 20 za vyakula vya mifugo ambapo kinategemewa kuzalisha ajira za watu zaidi ya 400.

Je Rais Magufuli Ktuachaje Kagera?

Rais Magufuli kabla hajaondok Kagera katuachia miradi itakayoendelea kuchochea ukuaji wa kiuchumi katika Mkoa, katika sekta ya usafiri na usafirishaji Rais Magufuli katuachai  kilomita 213 za barabara  kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara ya Rusahunga- Rusumo Km 92 kujengwa upya, Barabara ya Bugene- Kasulo Kilometa 120 kujengwa kwa kiwango  cha lami  Kilometa 60 kati ya Kilometa 120.

Zingine ni barabra ya kutoka Kyerwa kuelekea Wilayani karagwe Kilometa 110 itajengwa kwa kiwango cha lami kwa kilometa 50 kutokea Wilayani Kyerwa. Barabara inayoelekea katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kagera  Kilometa 10 kujengwa kwa kiwango cha lami na Barabara inayoelekea Katika Shule ya Sekondari Ihungo Kilometa moja kujengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Bukoba. Aidha, daraja la Kitengurelitakamilika ifikapo Juni 2021 kuziunganisha Wilaya za Karagwe na Missenyi kuendelea kuchochea ukuaji wa uchumi.

Rais Magufuli kauacha  ujumbe kwa wananchi  Kagera wakiongozwa na watendaji wa Serikali yake kuhakikisha wanachapa kazi kwa kujituma ili kuleta maendeleo ya haraka katika mkoa wa Kagera . Vile vile kuhakikisha huduma za kijamii kwa wananchi zinapatikana kwa wakati nazo ni kama maji, umeme, na  huduma za afya.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa