- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MATENGENEZO YA BARABARA MKOANI KAGERA CHINI YA WAKALA WA BARABARA VIJIJINI NA MIJINI (TARURA)
Mkoa wa Kagera kupitia Meneja Mkoa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) umesaini Mikataba ya matengenezo ya Barabara Katika Halmashauri za Wilaya nane za Mkoa wa Kagera Biharamulo, Muleba, Bukoba DC, Bukoba MC, Missenyi Karagwe, Kyerwa na Ngara.
Mikataba iliyosainiwa gharama yake jumla ni Shilingi bilioni 6,172,774,773 ambapo jumla ya kilometa 1,049.07 zitafanyiwa matengenezo ya aina mbalimbali kama Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami, Matengenezo ya kawaida, Matengenezo ya maeneo karofi, na Matengenezo ya muda maalum.
Aidha, Mikataba hiyo itahusisha ujenzi wa Makaravati 138, Madaraja 5 na ujenzi wa mifereji ya kuongozea maji Mita za Ujazo 4,108 pamoja na kung’oa mawe Mita za Ujazo 4,786. Mikataba hiyo ilisainiwa tarehe 2 Februari, 2018 na mwisho wa Mikataba yote ni Juni 31, 2018
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa