- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera unapatikana Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Tanzania. Makao Makuu ya Mkoa yapo katika Mji wa Bukoba umbali wa Kilometa 1500 kutoka Jijini Dar es Salaam. Mkoa wa Kagera unapakana na nchi ya Uganda kwa upande wa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa Magharibi, Mikoa ya Geita na Kigoma kwa upande wa Kusini. Pia Mkoa wa Kagera unapakana na Ziwa Victoria kwa upande wa Mashariki ambapo kwa ndani ya Ziwa hilo Mkoa unapakana na Mikoa ya Geita, Mwanza na Mara. Vile vile Mkoa wa Kagera uko Kusini mwa Ikweta kati ya Latitude 1 “00” na 2”45”. Mashariki mwa ‘Greenwich' katika Longitudi 30”25” na 32”40”
Karibuni katika Mkoa wetu wa Kagera ambako kuna fursa mbalimbali za Kiuchumi, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Elimu, Utamaduni na Utalii pamoja na nyingine nyingi ili kwa pamoja tuweze kuujenga uchumi wa Kagera na Taifa letu kwa pamoja. Kaulimbiu yetu ni:“ Kagera Kazi, Amani na Maendeleo.“
Asante kwa kutembelea Tovuti yetu ya Mkoa wa Kagera ambako utapata Taarifa nyingi kuhusu mkoa wetu aidha karibuni kwetu Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa,
KAGERA.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa